MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetoa wito kwa wanachama wake kuwa makini na matapeli ambao huwapigia simu kuwataka watoe fedha ili wapatiwe Huduma.

Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko huo Bi. Amina Mtingwa ametoa wito huo kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Tamasha la Tisa la Biashara linaloendelea kwenye viwanja vya Maisara ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 59 ya Mapunduzi Matukufu ya Zanzibar.

“Tunawasihi wanachama wetu wasikubali kupokea maelekezo yoyote kutoka kwa watu wasio wajua kwani Huduma zetu zinatolewa Bure.” Alisema Bi. Amina.

Alibainisha kuwa wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanachama wakiwemo wastaafu kuwa wamepigiwa simu na watu waliojitambulisha ni maafisa wa serikali wakitakiwa kutoka fedha ili waweze kurekebishiwa mafao yao jambo ambalo sio sahihi.

“Tungewashauri wanachama na wastaafu wetu endapo watahitaji ufafanuzi kuhusu malipo ya mafao mbalimbali wawasiliane na ofisi za PSSSF ambazo zinapatikana mikoa yote Tanzania Bara na Visiwanj.” Alisisitiza.

Alisema Mfuko umekuwa ukishirikiana na Mamlaka zinazosimamia mawasiliano ili kuwabaini watu hao na kutoka mfano tayari kuna visa 12 vilivyotokea Mwezi Desemba Mwaka jana 2022 vimeripotiwa kwenye Mamlaka husika ili kuwabaini wahalifu hao wa kimtandao.

Akizungumza kuhusu uhakiki wa wastaafu Afisa huyo Mwandamizi wa Matekelezo alisema, zoezi hilo ni endelevu ambapo Mstaafu anapaswa kujihakiki mara moja Kila mwaka.

Akifafanua Bi. Amina alisema Mfuko una wastaafu wapatao 150,000 ambao hulipwa mafao ya jumla ya Shilingi Bilioni 60 Kila mwezi.

Alitoa wito kwa wanachama wa PSSSF walioko kisiwani Zanzibar kutembelea katika banda la Mfuko huo ili kuhudumiwa.

Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko huo Bi. Amina Mtingwa(kulia) akimuhudumia mwanachama aliyetembelea banda la PSSSF kwenye Maonesho hayo.

AFISA Mwandamizi wa PSSSF Bi. Hazina Konde akiwahudumia Askari Polisi.

Meneja wa PSSSF Zanzibar Bi. Amina Kassim (kulia) akiwa na Afisa Matekelezo Mwandamizi Bi. Amina Mtingwa (katikati) wakizungumza na mwanachama aliyefika kwenye banda la PSSSF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...