-Ataka ujenzi Juni mwaka huu uanze, Serikali imeshatoa fedha...wananchi wanataka barabara
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ametoa maelekezo kwa
Meneja wa Wakala wa Brabara ( TANROADS) Mkoa wa Morogoro kuhakikisha
hadi ifikapo Juni mwaka huu ujenzi wa barabara ya kutoka
Ifikara kwenda Lupilo hadi Malinyi na nyingine inatoka pale Lupilo kwenda Mahenge.
Chongolo ameyazungumza hayo leo Februari 02, 2023 Wilayani Ulanga katika kikao cha shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro,ambapo amesema
baada ya kukagua ujenzi wa barabara inayotoka daraja la Kidatu kwenda
Ifakara ambapo mkandarasi yuko kazini na Oktoba mwaka huu itakuwa
imekamilika na tayari ameshazungumza na Meneja wa barabara Mkoa wa
Morogoro.
"Sasa hivi Mkandarasi anaonekana yuko barabarani lakini
tumekubaliana ikifika Oktoba suala la daraja la Kidato pamoja na hiyo
barabara iwe historia. Wakati nakuja huku leo asubuhi nimezungumza na
Rais Samia Samia Suluhu ameniuliza kuhusu barabara hiyo...
"Nikamwambia
tumekubaliana na Meneja wa barabara iwe imekamilika Oktoba mwaka
huu.Pia akaniambia alikuwa amewaagiza watangaze barabara ya kutoka
daraja la Kilombero kwenda Lupilo huko Malinyi na kwenda Mahenge na
tayari wameshatangaza tangu Oktoba ,2022 na kufungua zabuni.
"Ndugu
wananchi mmemsikia Meneja wa Barabara Mkoa wa Morogoro kwamba Serikali
ilishatoa fedha kujenga barabara kutoka Ifakara mpaka Lupilo na pale
Lupilo inagawanyika kwenda Malinyi na nyingine inatoka pale Lupepo
kwenda Mahenge barabara hii imeshatangazwa zabuni ambayo ilifunguliwa
tangu Novemba ,2022 , sasa hivi timu ya watalaamu inafanya tathimini ili
kumpata Mkandarasi wa kuijenga kwa kiwango cha lami.
Chongolo
amefafanua imeshatangaza zabuni na wamekubaliana lazima mpaka Juni
mkandarasi awe site na wananchi wanataka barabara sio maneno ya mchakato
,upembuzi yakinifu.Nani anajua?Watu wanataka barabara ianze kuchimbwa,
ijengwe ndio watu wataamini tunachokisema.
"Sasa tumekubaliana
mwezi wa Sita Mkandarasi awe Site aanze kujenga, wakati barabara
inayotoka Kidatu kuja Ifakara inakamilika tunataka kuona lami sasa sio
ya kuburuza buruza bali yenye hadhi. Mahenge ni Wilaya ya kihistoria,
Mahenge ndio iliyoigawa Kilombero ,ndio imeigawa Malinyi sasa hauwezi
kuwa mama unazaa watoto halafu wanapata raha wewe unapata shida.Mnazaa
mtoto anafikishiwa barabara nyie wenyewe bado sasa umeitwa Makao Makuu
ya nini ?
"Sasa tumekubaliana na hiyo barabara sio deni tena
watekeleze kwasababu fedha ipo ikiifika Juni tunatarajia kuona vifusi
lakini niseme ukweli barabara ujenzi wake sio sawa na kupanda mti
,ujenzi wake unautalaam mwingi ndio maana unaona kila hatua wanachimba
udongo wanaenda kupima na ili iitwe barabara inatakiwa utalaamu.
"
Watu wengi wanadhania mtu yoyote anaweza akajenga na hasa
tunapozungumzia barabara hii kubwa , barabara ambayo imeanzia pale
darajani ukienda mpaka Malinyi njiapanda pale ni kilometa 110 na kutoka
pale Malinyi Center ni kilometa 10 na kwa ujumla barabara urefu wake ni
kama kilometa 160 na ujenzi wa kilometa moja ni Sh.bilioni moja ,kwa
hiyo tunazungumzia Sh bilioni 200 ambazo ni fedha nyingi
"Serikali
imezitafuta imezitenga lazima ijiridhishe na mambo kadhaa la kwanza
itafute mkandarasi mwenye hadhi na uwezo unaoendana na aina ya barabara
tunayotaka kujenga. Kwa hiyo huwezi kuchukua mkandarasi yoyote na hatua
za kufuata kupata mkandarasi huyo lazima utangaze na Sheria inataka
ukitangaza huitangazi hapa ndani bali unatangaza duniani ili mwenye
uwezo,"amesema.
Awali wakati anazungumza na wananchi Chongolo
amewaomba waendelee kuiamini Serikali,waendeeeni kuiamini Chama Cha
Mapinduzi ambacho Rais Samia yeye ndio Mwenyekiti wake kwani
kimeidhamiria kutatua changamoto kwa kasi kubwa mpaka zote zikapokoma.
Aidha
amesema mwaka 2020 walipewa dhamana ya kuongoza nchi na kazi ya
kuongoza nchi haitaki uwe lele mama ni lazima uwe sawa sawa na wao(
CCM)kwasababu wanadhamana hiyo wametoka ofisini kushuka chini kwa
wananchi kuona nini kimefanyike na nini kilichoahidiwa na Kiko kwenye
hatua gani ya utekelezaji.
Nae Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM
Taifa itikadi na Uenezi Sophia mjema amesema ni muhimu kwa Wana CCM
kuuelezea Umma kuhusiana na Mafanikio ya Serikali kupitia Chama hicho,
hasa katika Utekelekezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, Uboresha
Sekta ya Afya, Elimu, Umeme, Kilimo pamoja na miundo mbinu mbalimbali.
"Niwasihi
Wana CCM kuwa kazi yenu kubwa ni kukisemea Chama cha Mapinduzi kutokana
mafanikio yaliyopatikana, Kuyazungumzia mazuri yaliyofanywa na Serikali
kupitia CCM chini ya Mwenyekiti wetu Dkt Samia Suluhu Hassan'" ameleeza
Mjema.
Kwa Upande wake Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa
Oganaizesheni, Issa Haji Gavu amewasisitiza Wana CCM na Wananchi wa
Ulanga kuwa na wajibu wa kulinda na kudumisha amani iliyopo, hatua
ambayo itakuwa kichocheo cha kuendelea kujileletea maendeleo na kufungu
zaidi milango kwa wawekezaji kutoka nje ya nchi.
Katibu mkuu wa
CCM, Daniel Chongolo anaendelea na ziara yake ya Siku 9 mkoani Morogoro
akiambatana na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi
Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa
Oganaizesheni Issa Haji Gavu.Katibu
wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akisisitiza jambo Mbele ya Wajumbe wa
chama hicho na Wananchi kwa ujumla kwenye mkutano uliofanyika kwenye
mkutano wa shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akizungumza mbele ya Wajumbe na
wananchi kwenye mkutano wa shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani
Morogoro.Chongolo ameongozana Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa
Itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri kuu ya
CCM Taifa Oganaizesheni Issa Haji Gavu.
Katibu
wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Meneja wa TANROADS mkoa wa
Morogoro Mhandisi Alinanuswe Kyamba alipokuwa akieleza maendeleo ya
ujenzi wa barabara mbalimbali ndani ya Wilaya ya Ulanga kwenye mkutano
wa shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro
Katibu
wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Sophia Mjema
akizungumza na Wajumbe pamoja na Wananchi kwenye mkutano wa shina namba
5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro
Katibu
wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Sophia Mjema akiteta
jambo na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Issa Haji
Gavu wakati wa mkutano wa Shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani
Morogoro
Mbunge
wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Salim Hasham akizungumza Mbele ya
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Danie Chongolo akiwasilisha mambo mbalimbali ya
maendeleo katika jimbo hilo kwa Wananchi kwenye mkutano wa shina namba
5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro
Wajumbe
wa mkutano wa shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro
wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo ambao Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Daniel Chongolo amehuduria akiwa sambamba na viongozi wengine
aliombatana nao kwenye ziara yake ya siku 9 mkoani Morogoro
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...