Waziri wa Nishati Januari Makamba akizungumza na wadau wa sekta ya Nishati Leo Februari 01,2023 Jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali waliojitokeza katika Mkutano wa Sekta ya Nishati Jijini Dar es salaam wakisikiliza hotuba ya waziri wa Nishati Januari Makamba na kuwataka wawekezaji watoe hofu nchi ya Tanzania ina amani na salama kwa uwekezaji.

Na Khadija Seif, Michuzi Tv
WIZARA ya Nishati yafungua rasmi Mkutano wa siku tatu wa Wadau wa Sekta ya Nishati nchini kutoka Mataifa mbalimbali Jijini Dar es salaam

Akizungumza na Wanahabari leo Februari Mosi, 2023 Waziri wa Nishati Januari Makamba wakati akifungua Mkutano huo kwa wa wawekezaji wa Sekta ya Nishati kutoka mataifa mbalimbali Jijini Dar es salaam amesema Serikali ipo tayari kuweka nguvu kwenye sekta binafsi kuhakikisha Sekta hiyo inatoa fursa mbalimbali.

Hata hivyo Makamba amewatoa hofu wawekezaji hao kuwa Taasisi ni nchi yenye Amani katika uwekezaji.

"Tumewakaribisha wawekezaji tupo tayari kuhakikisha uwekezaji wao unakuwa wenye tija zaidi hata hivyo serikali ipo tayari kuweka nguvu kwa sekta binafsi kwa maslahi mapana ya kupiga hatua za kimaendeleo nchini Tanzania. "

Pia ametoa wito kwa wadau wa sekta hiyo kushiriki Mkutano huo wa siku 03 ambao unatoa nafasi ya kujifunza vitu mbalimbali pamoja na kubadilishana uzoefu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya jumuiya ya watoa huduma katika Sekta ya Nishati na gesi Abdulsamad Abdulrahim amesema wadau ada wa sekta ya Nishati wametayarisha mkutano huo kwa kuona Tanzania ni nchi yenye amani na ina Kiongozi imara na shupavu pamoja na kuvutiwa na fursa zilizopo nchini.

"Tuna gesi nyingi na wawekezaji wengi wanakuja na hata wawekezaji hawa waliojitokeza kwenye Mkutano huu leo wameelezwa kuwa nchi hii imejaa fursa nyingi na inahitaji kupiga hatua kimaendeleo kupitia sekta ya Nishati mbadala na gesi.

Pia ameeleza kuwa waziri Kamba amewapa taarifa kuwa kuna miradi takribani 20 inatarajiwa kusainiwa siku za karibuni

"Inawapa wawekezaji imani kuwa kasi ya Wizara hiyo inapiga hatua kwa vitendo zaidi pia wawekezaji wanatamani kuona pesa zinafanya kazi katika miradi mbalimbali ipasavyo."

"Kuna wawekezaji wameonyesha mfano hai kuwa nchi zingine zimepiga hatua hivyo wametaka kueka ubia na nchi ya Tanzania na kuona inapiga hatua kubwa katika sekta ya Nishati.

Hata hivyo ametoa rai kwa viongozi mbalimbali kumpa ushirikiano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye juhudi zake za kuhakikisha Tanzania ina Maendeleo na wawekezaji kuendelea kuwekeza nchini Tanzania ili kuongeza ajira nyingi kwa wazawa .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...