Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amewataka vijana kushiriki kwenye sekta za uzalishaji mali hasa kilimo na ufugaji ili kutatua changamoto za ukosefu wa ajira na kipato miongoni mwa Vijana.
Mbunge Mavunde ameyasema hayo jana katika eneo la Mkombola-Hombolo wakati akikabidhi shamba hilo la ekari 5 kwa Vijana wa Dodoma Mjini ambalo litatumika kwa kilimo cha mboga mboga na matunda huku malengo makuu yakiwa ni kuihudumia Dodoma na mikoa nje ya Dodoma kwa mboga mboga na matunda.
“Shamba hili nililinunua miaka mingi ya nyuma nikiwa bado kijana mdogo mwenye ndoto za kilimo lakini leo nitafurahi ninyi mkiitimiza hii ndoto na maono yangu.
Nimeamua kuwakabidhi shamba hili ili sasa litumike kama sehemu ya kukuza uchumi wa Jumuiya yenu ya Vijana na mimi nikiwa kama mlezi wenu ninao wajibu wa kuhakikisha ninawasimamia ili muweze kujitegemea kiuchumi.
Eneo hili lina mkondo wa maji ambao haukauki hivyo mna uwezo wa kufanya kilimo kwa mwaka mzima pasipo changamoto yoyote.
Leo ninawakabidhi Shamba lenye ukubwa wa ekari 5,pampu ya maji na mpira mkubwa wa mita 100 pamoja na Rain gun sprinkler yenye uwezo wa kumwagilia mpaka umbali wa mita 30.Lakini naahidi kuwajengea na eneo ambao wasimamizi wa shamba wataishi.
Nataka kuwaona vijana wa Dodoma Mjini kupitia mradi huu mnabadilika na mnakuwa mfano kwa vijana wengi wa Tanzania.
Mwisho namshukuru sana Ndg. Ray Mark Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya kilimo ya Vijana ijulikanayo kama Young World Feeders kwa kukubali kutoa mafunzo ya kilimo kwa vijana bure kupitia shamba lake”Alisema Mavunde
Wakishukuru kwa niaba ya vijana,Mwenyekiti wa UVCCM Ndg. Shaban Shaban na Katibu wake Ndg. Isack Ngongi wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kushughulika na masuala ya vijana hasa katika kuwainua kiuchumi na kuahidi kusimamia kwa dhati mradi huu wa kilimo ili mwisho wa siku malengo yaweze kutimia ya uwezeshwaji wa vijana kiuchumi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...