Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Winga wa Kimataifa wa Ghana ambaye alikuwa anacheza katika Klabu ya Hatayspor Kulübü ya nchini Uturuki, Christian Atsu amefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi katika tetemeko la ardhi lililotokea nchini humo na nchi jirani ya Syria.

Kifo cha Atsu kimethibitishwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ghana mapema leo, baada ya Wizara hiyo kupokea taarifa kuwa mwili wa Mchezaji huyo umekutwa umefunikwa na kifusi katika nyumba yake ambayo alikuwa anaishi wakati yupo nchini Uturuki.

Hata hivyo, Atsu alikuwa anatafutwa kwa takribani siku 12 tangu kutokea kwa tetemeko hilo la ardhi, Februari 6, 2023 ambapo timu ya uokoaji inayoendelea na kazi hiyo ilifanikiwa kuona mwili wa Mchezaji huyo katika nyumbani hiyo aliyokuwa anaishi.

Mapema Februari 18, 2023 Ubalozi wa Ghana nchini Uturuki ukiwa chini ya mmoja wa Maofisa wa Ubalozi huo sanjari na ndugu zake marehemu Atsu, Kaka yake na Dada yake walifika katika eneo hilo ambapo mwili wake ulikutwa umefunikwa na kifusi hicho.

Kupitia mitandao ya kijamii, Klabu ya Hatayspor imethibitisha taarifa hizo za kifo cha Atsu, huku wakisema wanajiandaa kusafirisha mwili wake kuelekea nchini Ghana kwa ajili ya mazishi, sanjari na kusikitishwa na kuondokewa na Mchezaji huyo muhimu katika Kikosi chao.

Serikali nchini Ghana imetoa salamu za pole kw
a ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa marehemu baada ya kutokea kifo hicho, hata hivyo Ubalozi wa Ghana nchini humo unaendelea na taratibu za kusafirisha mwili wa Atsu kwa ajili ya mazishi nchini Ghana.

Christian Atsu enzi za uhai wake amewahi kucheza Klabu za FC Porto ya Ureno, Chelsea na Newcastle United za Uingereza, amekutwa na umauti katika janga hilo la tetemeko la ardhi lililotokea katika nchi za Uturuki na Syria na kusababisha idadi kubwa ya watu kupoteza maisha.


REST IN PEACE, CHRISTIAN ATSU.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...