Na Khadija Seif, Michuzi TV
MDHAMINI wa mapambano ya ngumi nchini kwa upande wa vifaa na tiba Roby One Pharmacy amehaidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa mapambano mbalimbali mwaka huu wa 2023, likiwemo pambano la ‘Queen of Boxing’ litakalofanyika Machi 11, 2023 katika ukumbi wa Ubungo plaza jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Michuzi Blog, Mkurugenzi wa Robby One Pharmacy, Robert Mchunguzi amesema waandaaji wa pambano la ‘Queen of Boxing’ wametoa fursa hiyo na kuwapa nafasi kubwa mabondia wanawake kuonekana na wao kama wadau wa ngumi nchini watashiriki kikamilifu kwenye pambano hilo.
“Tumezoea kuona mabondia wa kike wakipewa nafasi ndogo au chache kwenye mapambano makubwa ambayo mara nyingi tunawaona kwenye mapambano ya utangulizi lakini ‘Queen of Boxing’ ni pambano kubwa likihusisha .abondia wanawake pekee,” amesema Mchunguzi
Aidha, Mchunguzi amesema kutokana na ujio wa mapambano hayo ya ‘Queen of Boxing’ wao Robby One wataendelea kushirikia na kushirikiana na mratibu mapambano hayo hadi kufika mwisho wake.
Mchunguzi amesema: “Nitashirikiana na Mratibu wa pambano hili pale atakapo kwama kwa upande wa Dawa na Vifaa tiba kwa ajili ya Mabondia, sisi Roby One Pharmacy tutakuwa nao bega kwa bega.”
Kwa upande wake Promota wa pambano hilo, Dk Khadija Hamisi amesema kutakuwa na mapambano nane na shughuli nzima itafanyika Ubungo Plaza Machi 11, 2023.
Aidha amesema bondia Stumai Muki atapigania mkanda wa ubingwa wa UBO dhidi ya Chimwemwe Banda kutoka Zimbambwe uzito wa KG 52 katika raundi nane.
Dkt. Khadija amewaomba Wanawake hususani wanamichezo kujitokeza kwa wingi siku ya Wanawake Duniani ambapo huadhimishwa kila ifikapo Machi 8, hivyo wataitumia siku hiyo kujumuika na wanawake wa kitanzania katika kupima afya kwa magonjwa mbalimbali kwa hiari katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Mabondia ambao watapanda ulingoni Machi 11,2023 katika pambano la 'Queen of Boxing ' linalotarajiwa kufanyika Ubungo plaza Jijini Dar es salaam ambapo kulia ni bondia Happy Daudi kushoto kwake bondia Najma isike wakiwa na Mkanda wa TPBRC ambao Bondia kutoka Tanzania Stumai Muki pamoja na Chimwemwe Banda kutoka Malawi wataugombania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...