Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Pilsner Lager imefanya droo ya kwanza ya promosheni yake pendwa ijulikanayo kama ‘Kapu la Wana’ kubainisha washindi wa kwanza wa promosheni hiyo ambayo ni maalumu kwa wateja wa bia hiyo wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini.
Kupitia promosheni
hiyo inayofanyika kwa muda wa wiki 8, wateja wa bia ya Pilsner
watajishindia zawadi mbalimbali zikiwemo, televisheni, simu janja,
pikipiki na zawadi ya mwisho ya gari. Droo iiliyofanyika jana,
walipatikana washindi 7 kutoka kanda zote tatu, ambapo mshindi mmoja
kutoka kanda ya Ziwa alishinda pikipiki, wengine watatu kutoka kanda
zote tatu walishinda simu janja na wengine watatu walishinda
televisheni. Washindi hao wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao tarehe 18
mwezi huu.
Washindi walioshinda simu janja ni Agatha Mvwango, Eli
Elias na Hassan Joel; waliojishindia television za kisasa ni Justine
Mwaipaja, Neema Abdallah na Selina Panga. Na mshindi wa bodaboda ni
Neema Mathias kutoka kanda ya Ziwa.
Akizungumza wakati wa droo
hiyo, Meneja wa bia ya Pilsner, Wankyo Marando alisema, droo hiyo ni
mwanzo tu wa promosheni ya ‘Kapu la Wana’, akitoa wito kwa wateja wa bia
ya Pilsner mikoa ya kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini kuendelea
kushiriki kwenye promosheni hiyo kwani zawadi ni nyingi.
“Kupitia
promosheni hii tunawazawadia wateja wetu wachapa kazi, na zawadi zipo
nyingi sana hivyo nawatia moyo wateja wetu wa mikoa ya hizi kanda tatu,
yani kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini waendelee kununua bia ya
Pilsner, wapate kadi ya kukwangua, wakipata namba wataituma kupitia
ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa namba 15320 baaada ya hapo watapokea
ujumbe mfupi kudhibitisha ushiriki,“ alisema Marando.
Kwa upande
wake, Muwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ya Tanzania,
Salim Mgafi aliwapongeza washindi wa droo hiyo ya kwanza kwa njia ya
simu, na pia alipongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa kufanya
promosheni kwa kufuata kanuni na taratibu za bodi ya Michezo ya
kubahatisha.
Hii ni mara ya pili bia ya Pilsner imekuja na
promosheni hii ya ‘Kapu la Wana’ na imetenga zaidi ya Tsh. 36 milioni
kwa washindi 22 wa kampeni hiyo.
Menaja wa bia ya Pilsner, Wankyo Marando (Kulia) kutoka kiwanda cha bia cha Serengeti, akizungumza kwa njia ya mtandao na washindi wa droo ya kwanza wa promosheni ya bia hiyo ijulikanayo kama ‘Kapu la Wana’, iliyofanyika Dar es Salaam jana ambapo wateja saba wa bia ya Pilsner walijishindia televisheni za kisasa, simu janja na pikipiki moja. Kushoto ni muwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Salim Mgafi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...