Na.Vero Ignatus,Arusha
Waziri
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na
Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama (Mb) ameagiza Taasisi zote za umma
ziwajibike kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na kama kuna
mahali hawatumii wajitathmini,ili kupunguza urudufu wa uhitaji wa kila
Taasisi ya Umma kuwa na mfumo wake.
Mhagama ameyasema hayo
kwakati wa kufunga kikao kazi cha tu cha Serikali Mtandao Jijini Arusha,
kuwa wapo wataalam wengi wanaotumia huduma za Kidigitali ambapo
amewataka kuwa Wazalendo kwa Taifa sambamba na kuwataka kwenda kufanya
thamini kwenye utendaji wao.
"Kuna baadhi ya wataalam wanaotumia
huduma hizi za kidigitali kwa kunyofoa baadhi ya vitu kwenye mfumo
mkongo wa Taifa, lakini hawana uzalendo kwa Taifa,ukishaambiwa mtandao
upo chini ujue ukiona manyoya ujue ishaliwa
Watumishi wa umma tuongozwe na uzalendo kwa taifa ketu,nendeni mkafanye tathmini katika utendaji wetu" alisema Mhagama
Mhagama
ameziaagiza Taasisi za Umma/Serikali kutekeleza maazimio yote
yalioyopitishwa 12 kwenye kikao kazi cha siku 3 cha Serikali Mtandao
(eGA)huku akiwataka kwenda kuyatumia kama kichocheo kikubwa cha kujenga
ufanisi yatakayoendana na mabadiliko ya kasi ya teknolojia.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa EGa Mhamdisi Benedict Ndomba alisema kuwa
Kikao kazi hicho kimekuwa cha manufaa makubwa kwani wameweza kukaa na
kujadiliana kwa pamoja namna ya kuweka mikakati na yakimkakakati namna
ya kutatua changamoto na kuzigeuza kuwa fursa ambapo washiriki 1624
waliweza kuhudhuria
Aidha amesema wamepokea maagizo ya mhe.
waziri na kuahidi kwenda kuyatendea kazi sambamba lile la Taasisi idara
na vitengo kujitahidi kutenga bajeti ya mafunzo pamoja na kuhakiiisha
kuwa mafunzo hayo yanafanyika na haswa mifumo ya kukusanya mapato ya
serikali
Wametoa ahadi kwamba wanakwenda kuhuisha tovuti zao
na kuhakikisha kuwa taarifa zao kwmaba ni sahihi na kuhakikisha
wanakwenda kufanya kazi kidigitali pampja na vikaonvyote vyankisheria
vinakwenda kutekelezwa kidigitali
Katibu wa Viziwi tawi la Mkoa
Pwani Suleiman Zalala (Chavita)aliyepata mualiko katika kikaokazi hicho
cha siku tatu ameishukuru Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa kuwashirikisha
katika kikao kazi hicho na wamewaomba taasisi nyingine kutowasahau
katika shughuli zao za kila siku
Mamlaka ya Serikali Mtandao ni
taasisi iliyoanziahwa kwa sheria ya serikali Mtandao Na 10 mwaka
2019,ikiwa na majukumu ya kuratibu,kusimamiana na kukuza jitihada za
serikali ,pamoja na kusmamia uzingaiaji wa sera,sheria,kauni naviwango,
aambapo inaendeleza afua za wakala ya Serikali Mtandao iliyoundwa Aprili
2012 kwa sheria ya Wakala za serikali no.30 sura ya 245 ya mwaka 1997.
Kabla
ya kuanzishwa kwa Wakala y Serikali Mtandao,matumizi ya TEHAMA
serikalini yalikuwa yanaratibiwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais
Menejimenti yaa utumishi wa Umma na Utawala Bora chini ya Idara ya
Usimamizi wa Mifumo (DMIS)ambayo kwa sasa ni Idara ya Huduma za TEHAMA
Serikalini (DICTS)
Aidha Mamlaka hiyo inaongozwa na misingi mikuu
sita ambayo inaekekeza kuhusu tabia na mwenendo wa watumishi wake kwa
ngazi zote ambayo ni: Uadilifu,Ubunifu,Kuthamini wateja,Ushirikiano
pamoja na weledi.


Pichani ni wajumbe wa kikao kazi cha tatu cha Serikali Mtandao kikiwa kinahitimishwa na Mhe.Mhagama kilichofanyika katika ukimbi wa kimataifa wa AICC
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...