Na Mwandishi wetu, Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum imeanza kuangalia uwezekano wa kuondoa dhamana kwenye makosa ya ulawiti na ubakaji ili kukomesha vitendo hivyo vilivyokithiri nchini. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi ameyasema hayo bungeni leo Februari mosi, 2023 alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Judith Kapinga kwa niaba ya Wizara ya Katiba na Sheria. Katika swali lake, Mbunge huyo amehoji serikali ina mkakati gani wa kurekebisha sheria ya ubakaji na ulawiti wa watoto ili kuwe na kifungu tofauti cha sheria.

 Akijibu swali hilo, Mhe.Katambi amesema kukithiri kwa vitendo hivyo hakutokani na mapungufu kwenye sheria na kwamba uthibitishaji wa makosa ya jinai unatakiwa kufanyika bila kuacha shaka yeyote lakini ushahidi huharibiwa wakati wa upelelezi. Naibu Waziri Katambi amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliona hilo na kuunda Tume maalum ya haki jinai.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...