

Mkurugenzi wa Elimu Maalum wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Magreth Matonya akizungumza kuhusiana na nchi ya Tanzania ilivyokabiliana na UVIKO 19 katika Mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa elimu wakifatilia mada katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan jjjini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa Canada Helen Fyche na watendaji waandamizi wa Taasisi ya Maendeleo ya Aga Khan pamoja na Watendaji wa Nchi za Kenya, Tanzania na Uganda, Jijini Dar es Salaam.
*Profesa Mtenzi adai mifumo ya elimu iliharibika katika kipindi cha UVICO 19.
Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv
TAASISI ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan imekutana na wadau wa elimu wa nchi tatu za Tanzania, Kenya pamoja na Uganda kujadiliana mifumo ya elimu ya kukabiliana na majanga baada ya kupita katika janga la UVIKO 19.
Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa wadau wa elimu katika nchi za Afrika Mashariki uliofanyika nchini Tanzania Mwakilishi wa Balozi wa Canada Helen Fyche amesema kuwa Taasisi ya Elimu ya Aga Khan imefanya utafiti na kutaka kubadilishana uzoefu namna elimu ilivyo kumbwa na mtikisiko wa UVIKO 19 na kila nchi ilivyoweza kukabili pamoja na kuweka mikakati ya majanga mengine yakitokea.
Fyche amesema nchi ya Canada inashirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ikiwemo elimu katika kujenga mazingira bora ya kusomea pamoja na ujuzi wa kuandaa walimu bora kwenye vyuo ikiwemo Chuo cha Elimu Kigoma.
Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan Profesa Jane Rarieye amesema kuwa Taasisi imeweka kipaumbele cha walimu hivyo UVIKO 19 iliathiri walimu ambapo walimu wanatakiwa kuangaliwa kwa umhimu kwani katika kuendeleza elimu lazima walimu wakae katikati.
Amesema wakati wa UVIKO 19 shule zilifungwa kwa wanafunzi kukaa nyumbani baada ya kutengamaa na wanafunzi kurudi baadhi hawakurudi kwa kwenda kutafuta njia nyingine za kuishi kutokana na baadhi ya familia kupoteza wazazi.
Profesa Jane amesema Taaisi ya Elimu ya Aga Khan ina mradi ambao utakwenda kufundisha wakuu wa shule pamoja na wakuu vyuo namna ya kuweza kukabili majanga mengine yakitokea bila kuwaacha walimu ambao ndio nguzo katika jambo lolote la elimu.
Mkurgenzi wa Elimu Maalumu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk.Magreth Matonya amesema kuwa katika kipindi cha UVICO Tanzania ilipata changamoto ya kutumia Tehama pamoja na kuwafikia elimu
Amesema Wizara imeweka mikakati ya kukabili majanga kwenye sekyta namna ya kuelimisha walimu na wanafunzi na namna ya kuweza kufikisha taarifa pindi majanga yakatayotokea.
Dkt.Matonya amesema katika kipindi cha changamoto ya mawasiliano kwa watoto wasio ona na pamoja na wasiosikia na wale wanaotumia baskeli ya miguu mitatu.
Amesema kuwa wakati wa UVICO 19 Serikali ilijenga zaidi ya madarasa ya zaidi ya 15000 kwa ajili ya kutoa nafasi baina ya mwanafunzi na mwanafunzi katika kukabili maambukizi ya ugonjwa huo pamoja na kujenga Studio itakayotumika kunakiri sauti kwa ajili ya kufundishia.
Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi wa Wizara ya Elimu ya Nchini Kenya Nerreel Olicis amesema kuwa mkutano wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan juu ya kujadiliana yale yaliyotokea katika kipindi cha janga la UVICO 19 ambapo kwa nchi ya Kenya imekuja na mtaala wa ujuzi na maarifa ya namna ya kutoa elimu bora kwa wanafunzi.
Amesema wakati wa UVIKO 19 Kenya ilifunga shule kwa miazi nanne hivyo wangekuwa na mpangilio wa maandalizi ya kukabili majanga wanafunzi wangesoma lakini halikuweza kufanyika.
Amesema Taasisi ya Aga Khan inafundisha walimu hivyo kwa ushirikiano huo utajenga elimu bora na kujiandaa na majanga mengine pandi yanapotokea.
Olicis amesema kuwa kilichofanyika ni pamoja kuwa vitabu kwa wanafunzi kutoka shule ya msingi hadi sekondari hii ambayo wanafunzi wanakaa navyo kuweza kusoma kila mada zilizomo na kuweza kujibia hata mitihani kwa wakati mwingine wa majanga.
Mkuu wa Utafiti wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Profesa Fredrick Mtenzi amesema mkutano huo ni baada ya Korona mifumo ya elimu ilivurugika na kile kilichoonekana ni namna ya kutoa elimu
Amesema kuwa kwa sasa tunatakiwa na kujiandaa kwa kuhakikisha walimu wanajengewa uwezo pamoja na wanafunzi kuweza kusoma katika mifumo mingine ikiwemo na kutumia Tehama
Amesema kuwa Tanzania walifanya ufafiti katika Mkoa wa Lindi pamoja na nchini Uganda ambapo kwa sasa nchi zote zimefika kwa kujadiliana na kubadilishana uzoefu kwa kile walichopitia kwenye janga la UVIKO 19.
Amesema kuwa katika tafiti walichokiona ni jambo moja muhimu ni walimu ndio watu mhumu wa kujengewa uwezo namna ya kuweza kuendelea kufundisha wanafyunzi wakiwa nyumbani wakati nchi zikiwa zinapita katika majanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...