Benki ya Exim Tanzania imezindua kampeni yake ya upandaji miti 10,000 katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini hususani mikoa Arusha na Kilimanjaro ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa mkakati endelevu wa benki hiyo unaofahamika kama ‘Exim Go Green Initiative’ unaolenga kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Sambamba na zoezi hilo la upandaji miti benki hiyo pia ilikabidhi msaada wa jumla ya ndoo za kuhifadhia takataka (waste bins) 100 katika mikoa hiyo ili kusaidia uhifadhi wa takataka mbalimbali zinazozalishwa katika maeneo mbalimbali ya miji hiyo.
Walikuwa ni viongozi waandamizi wa benki ya Exim Tanzania akiwemo Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu Benki hiyo Bw Fredrick Kanga na Ofisa Mkuu Idara ya Fedha Bw Shani Kinswaga walio ongoza uzinduzi wa kampeni hiyo kwa nyakati tofauti kwa kukabidhi msaada wa ndoo hizo pamoja na kupanda miti katika hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro, hospitali ya Wilaya ya Karatu pamoja na shule ya wasichana ya Arusha iliyopo mkoani Arusha.
“Kimsingi ni kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanayochangiwa na kukua kwa shughuli za kibinadamu hivyo jamii isipopambana na kuidhibiti hali hiyo kwa kupanda miti na kuacha kuharibu mazingira jangwa na maafa vitazidi kutokea.’’
“Benki ya Exim tumekuwa wadau wakubwa katika kuendesha kampeni za namna hii, baada ya kushikiriki kwenye jitihada hizi mikoa Dodoma sasa tumehamia mikoa hii ya Kaskazini na lengo ni kupanda miti 10,000 katika mikoa hii ambapo kwa kuzindua tu tumepanda jumla ya miti 600 katika mikoa yote miwili. Zaidi pia tumetoa msaada wa jumla ya ‘waste bins’ 100 katika mikoa hii,’’ alibainisha Bw Kinswaga
Akizungumzia kampeni hiyo Bw Kanga alisema mikoa hiyo ya Kaskazini ni moja ya mikoa ambayo kwasasa inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi yanayochangiwa shughuli za kibinadamu hususani ukataji miti na ukuaji wa sekta ya viwanda ambao unasababisha ongezeko la gesi ukaa hali inayosababisha ukosefu wa mvua za kutosha na zisizotabilika na ongezeko la joto.
“Kwa ujumla hali siyo ya kuridhisha sana, sisi sote ni mashahidi wa namna hali hii inavyo athiri mustakabali wa urithi wetu tunaojivunia kwa miaka mingi yaani Mlima Kilimanjaro.”
“Zaidi pia changamoto ya uhaba wa mvua imekuwa ikisababisha mavuno hafifu hali ambayo pia inasababisha kuzorota kwa uchumi. Kama inavyofahamika sisi kama taasisi ya kifedha tunaguswa moja kwa moja na athari za kiuchumi na ndio sababu tunaamua kujiingiza moja kwa moja kwenye jitihada kama hizi.’’ Alisema.
Wakitoa nasaha zao kwa nyakati tofauti viongozi waandamizi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa hatua hiyo walisema kwa kiasi kikubwa wanaridhishwa namna wadau mbalimbali ikiwemo benki hiyo wanavyoendelea kushirikiana na Serikali pamoja na mamlaka zake katika kufanikisha jitihada zinazoendelea kitaifa zakutangaza kutunza mazingira kupitia mipango mbalimbali ya uwajijbikaji kwa jamii.
“Inatia moyo kuona kwamba jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali kulinda mazingira zinaungwa mkono na wananchi na wadau kama benki ya Exim. Nawapongeza sana benki ya Exim Tanzania kwa kubuni mpango huu wa Exim Go Green Initiative ambao naamini utaendelea kuwa na tija kubwa katika utunzaji wa mazingira katika maeneo mbalimbali hapa nchini.’’ Alisema Bw Abel Ntupwa , Ofisa Elimu Mkoa wa Arusha aliemuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Bw John Mongella katika uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu Benki ya Exim Bw Fredrick Kanga (wa nne kushoto) akikabidhi msaada wa ndoo za kuhifadhia takataka (waste bins) 50 kwa Afisa Elimu Mkoa wa Arusha Bw Abel Ntupwa (wa tatu kulia) pamoja na miche ya miti, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 10,000 inayoendeshwa na benki hiyo katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini hususani Arusha na Kilimanjaro ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa mkakati endelevu wa benki hiyo unaofahamika kama ‘Exim Go Green Initiative’ . Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni kwenye viunga vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Arusha. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mheshimiwa Maximilian Iranghe (wa pili kulia), maofisa waandamizi Benki ya Exim, walimu na wanafunzi wa shule hiyo

Ofisa Mkuu Idara ya Fedha benki ya Exim Bw Shani Kinswaga (wa sita kushoto) akikabidhi msaada wa ndoo za kuhifadhia takataka (waste bins) 25 kwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bw Bw Dadi Kolimba (alievaa kofia ) ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 10,000 inayoendeshwa na benki hiyo katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini hususani Arusha na Kilimanjaro ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa mkakati endelevu wa benki hiyo unaofahamika kama ‘Exim Go Green Initiative’ . Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni kwenye viunga vya Hospitali ya WIlaya ya Karatu. Wanaoshuhudia ni pamoja na viongozi wa chama na serikali wilayani humo pamoja na maofisa waandamizi wa benki hiyo.

Mkuu wa Matawi ya Exim kanda ya Kaskazini, Bw Amos Lyimo (wa nne kushoto) akikabidhi msaada wa ndoo za kuhifadhia takataka (waste bins) 25 kwa Mkuu wa uongozi wa Hospitali ya Mawezi mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 10,000 inayoendeshwa na benki hiyo katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini hususani Arusha na Kilimanjaro ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa mkakati endelevu wa benki hiyo unaofahamika kama ‘Exim Go Green Initiative’ . Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni kwenye viunga vya Hospitali ya Mawenzi mkoani humo. Wanaoshuhudia ni pamoja na viongozi wa hospitali hiyo pamoja na maofisa waandamizi wa benki hiyo.
Afisa Elimu Mkoa wa Arusha Bw Abel Ntupwa (alieshika koleo) akipanda mti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 10,000 inayoendeshwa na benki hiyo katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini hususani Arusha na Kilimanjaro ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa mkakati endelevu wa benki hiyo unaofahamika kama ‘Exim Go Green Initiative’ . Uzinduzi huo ulifanyika hivi karibuni kwenye viunga vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Arusha. Wanaoshuhudia ni pamoja na viongozi wa mkoa huo, maofisa waandamizi Benki ya Exim wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu Benki ya Exim Bw Fredrick Kanga ( wa tatu kushoto) , walimu na wanafunzi wa shule hiyo.


Zoezi la upandaji miti likiendelea katika Hospitali ya Mawenzi Mkoani Kilimanjaro, Karatu na Arusha.
“Inatia moyo kuona kwamba jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali kulinda mazingira zinaungwa mkono na wananchi na wadau kama benki ya Exim. Nawapongeza sana benki ya Exim Tanzania kwa kubuni mpango huu wa Exim Go Green Initiative ambao naamini utaendelea kuwa na tija kubwa katika utunzaji wa mazingira katika maeneo mbalimbali hapa nchini.’’ - Bw Abel Ntupwa , Ofisa Elimu Mkoa wa Arusha

Exim Go Green Initiative! Exim safi …mazingira safi!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...