Mwanzilishi
na Mkurugenzi Wa Kampuni Ya NALA , Bw. Benjamin Fernandes (katikati )
akionesha leseni ya mtoa huduma kwa malipo kutoka Benki Kuu ya Tanzania
mara baada ya kukabidhiwa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
mapema leo katika Hoteli ya Hyatt Jijini Dar Es Salaam. Kulia kwake ni
Meneja Bidhaa Thomas Robinson na kushoto ni Mtaalamu wa Progamu Bertha
Sanga .
Mtaalamu wa Progamu Bertha Sanga .akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari mara baada kukabidhiwa leseni ya mtoa huduma kwa malipo kutoka
Benki Kuu ya Tanzania mara .
NALA,kampuni ya Kitanzania inayowezesha huduma ya kutuma na kupokea
fedha kwa njia ya kidigitali sehemu mbali mbali duniani, imepata leseni
ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuahidi kuwekeza Dola za Kimarekani
milini moja, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 2.
Leseni ya BoT inaifanya NALA kuwa mtoa huduma ya malipo na kuwezesha muunganiko wa moja kwa moja na benki pamoja na waendeshaji wa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu za mkononi, kama vile Mpesa, TIGOPESA, Airtel Money na nyinginezo. Akiongea na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NALA Benjamin Fernandes alisema uwekezaji huo utaifanya NALA kuboreha huduma na kuongeza wigo wa huduma zake huku wateja wengi zaidi wakinufaika.
Fernandes
alisema hiyo itaiwezesha NALA kuanza kutengeneza bidhaa za ziada za
kidijitali ambazo zitaongeza ujumuishaji wa malipo, kufanya huduma za
malipo ziwe nafuu zaidi na za kuaminika kwa biashara na matumizi ya
kawaida. “Kwa kutumia NALA wateja wanaweza kutuma na kupokea fedha kwa
nia ya kijigitali kutoka nchi mbali mbali duniani ikiwa ni pamoja na
Marekani, Uingereza, nchi za Jumuiya ya Ulaya na nginginezo,” alifafanua
Mkurugenzi
huyo aliafafanua kuwa mara baada ya NALA kuzinduliwa katika Umoja wa
Ulaya, kampuni hiyo imepokea leseni yake ya mtoa huduma za malipo nchini
Tanzania na kuongeza kuwa hiyo ni hatua kubwa kwa kuwa inatoa nafasi ya
kuboresha huduma na kuongeza huduma mpya, kama vile; malipo ya
kibiashara, huduma za wafanyabiashara na malipo ya nje kutoka Tanzania,
pamoja na ushirikiano wa moja kwa moja na benki za ndani na kampuni za
mawasiliano.
Leseni hii imetolewa, ikiwa ni muendelezo wa juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwainua vijana, lakini pia kuweka mazingira rafiki ya kiuwekezaji kwa ujumla, ili makampuni mengi kama NALA yaweze kuwekeza nchini. Fernandes alisema “Malengo mawili makubwa ya NALA kutokea mwaka jana yamekuwa kuwezesha ushirikiano wa moja kwa moja kwa benki na kampuni za mawasiliano ya simu, kukabiliana na changamoto ambazo wafanyabiashara wanakabiliana nazo katika kuhamisha fedha kuvuka mipaka ya nchi.
Tumefanya kazi kwa karibu pamoja na Benki Kuu ya Tanzania ili kukamilisha hatua zinazofaa za kupokea leseni yetu kama mtoa huduma wa malipo. Kwa leseni hii mpya mkononi, NALA inapata nafasi na uwezo wa kuendelea na malengo yetu, kubwa likiwa kufanya uwekezaji wenye thamani ya zaidi ya Bilion 2 za kitanzania ili kujenga miradi yetu mikubwa zaidi kuwahi kutokea katika soko letu la hapa nyumbani Tanzania” NALA inapatikana nchi nyingi za Ukanda wa Afrika na Ulaya, unaweza kuipakua kwenye simu yako kupitia App Store au Play Store.
Licha ya chaguzi nyingi za kutuma pesa Afrika kutoka ng'ambo, bara hili bado limeendelea kuwa mahali pa gharama kubwa zaidi kutuma pesa. Benki ya Dunia inakadiria wastani wa ada za kutuma fedha Afrika kuwa 9%. Zaidi ya hayo, chaguo nyingi zilizopo ni pamoja na ada zilizofichwa ambazo hufanya iwe vigumu kutambua gharama halisi ya kutuma pesa.
NALA inajitahidi kubadilisha dhana ya zana za kifedha kwa Waafrika kwa kutoa huduma za haki na uwazi ili kuwawezesha watu kudhibiti fedha zao. Kuhusu NALA: NALA ni kampuni ya malipo ya Kiafrika na programu ya kutuma pesa ambayo hukuwezesha kufanya malipo salama na ya kuaminika kutoka Ulaya, Uingereza na Marekani hadi Afrika kwa sekunde chache.
Kampuni hiyo ina dhamira ya kuongeza fursa za kiuchumi katika bara la Afrika na miongoni mwa wanadiaspora duniani kote. Kuunda masuluhisho ya kifedha yanayoendeshwa na jumuiya, hurahisisha kufanya malipo ya kila siku na kuongeza fursa za biashara katika Afrika inayokua duniani. Malipo barani Afrika yamejengwa kwa 1%.
NALA
inatamani kuleta teknolojia ya malipo ya karne ya 21 barani Afrika ili
kuunda njia za malipo za gharama ya chini na zinazotegemeka sana ambazo
marafiki, familia na wafanyabiashara wanaweza kutumia. Ikiwa malipo ni
rahisi, ya kuaminika, na yanapatikana kwa kugusa kitufe, chochote
kinawezekana. Kwa
kujenga njia za malipo na miundombinu, NALA itawezesha malipo ya haraka
kwa bara la Afrika. Teknolojia yao imeundwa na wahandisi wa kiwango cha
kimataifa kutoka duniani kote na tunajivunia kuhudumia jumuiya zote,
kuanzia miji yenye shughuli nyingi hadi vijiji vyenye amani.
Tumebahatika kushirikiana na jumuiya hizi katika safari hii pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...