*TAGCO
yampa tuzo Rais Samia
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Maafisa
Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali wanao wajibu wa kuhakikisha wanatoa taarifa
za jinsi serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan ndani ya kipindi cha miaka miwili imefanya.
Mhe.
Majaliwa ameyasema hayo wakati akifungua Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) kwenye Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam Machi 27, 2023
“Maafisa
Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini, mnao wajibu wa kuhakikisha mnatoa
taarifa za jinsi serikali ilivyotatua shida hizo za wananchi kwani kwa
kutofanya hivyo wapo watu wengine wataendelea kufanya upotoshaji wakati sisi
wanahabari tunajua kuwa huo ni upotoshaji.”” Alifafanua.
Alisema
jukumu la kuisemea serikali ni moja ya sehemu ya mawasiliano ya nje ya serikali
kwahivyo wanapaswa kuzingatia.
Alisema
sambamba na hilo, aliwataka wanahabari wote wa serikali na binafsi wahakikishe
wananchi wanapata elimu na taarifa
sahihi kuhusu faida na umuhimu wa miradi na mipango au shughuli zinazotelekezwa
na serikali ikiwa ni pamoja na kuwapa taarifa sahihi kwa urahisi zaidi na kwa wakati.
Aidha
aliwataka wazingatie suala la uhuru wa kupata na kutoa habari unaoendelea
kutekelezwa kwa mujibu wa sheria, Taratibu na kanuni na wadau wote kila mmoja atimize
wajibu wake.
Pia
aliwataka kushiriki kikamilifu kuitangaza vema Tanzania ndani na nje ya nchi
hususan sula la amani na utulivu, fursa za biashara na uwekezaji, historia ya
nchi na kuweka msisitizo katika kufuata maadili na mila za nchi na kutangaza
mali kale na vivutio
Aidha
aliwataka kuweka mbele uzalendo, uadilifu, uhuru na maslahi ya nchi ili
kulijenga taifa na aliwakumbusha kuongeza ubunifu wa kusukuma ajenda za
serikali kwa umma.
Hali
kadhalika aliwataka kujiendeleza ili kuendana na asi ya mabadiliko ya
kiteknlojia.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia
ya Habari, Mhe. Nape Nnauye alisema Kikao hicho ambacho kimewaleta pamoja
Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali kutoka Bara na Visiwani ni muhimu kwa ustawi na mchango wa kada hii
katika utekelezaji wa shughuli za kila siku za serikali.
“Kikao hichi kitatumika pamoja na mambo mengine kutathimini mchango wetu katika kusukuma ajenda mbalimbali za serikali na namna ya kuboresha mchango huo.” Alifafanua Mhe. Nnauye.
Katika hatua nyingine TAGCO kimempa tuzo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua
na kuthamini mchango wake katika kuimarisha sekta ya habari, demokrasia, uwazi,
uhuru wa kutoa maoni na kupata taarifa nchini.
Tuzo
hiyo imepokelewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa kwa niaba ya Rais.
Akikabidhi
tuzo hiyo kwa niaba ya TAGCO, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari, Mhe. Nape Nnauye alisema, “Sisi maafisa habari serikalini,
tumemwelewa, tunamwamini na tunamuunga mkono kwa dhati, Anaishi anayoyasema na
anayatenda kwa ustadi mkubwa.” Alisema Mhe. Nape
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Mawasiliano ya Kimkakati Injini ya Maendeleo".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...