Afisa Mtendaji Mkuu wa Jubilee Allianz General Insuarance (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 28,2023, wakati wa uzinduzi wa bima ya mazao kuwakinga wakulima na hasara zinazosababishwa na majanga ya asili pamoja na mabadiliko ya tabia nchi, Kutoka kushoto ni Meneja Masuluhisho ya Kidijitali wa kampuni ya mbolea ya Yara, Deodath Mtei, Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Equity, Isabela Maganga na Mkurugenzi Mkuu wa Yara Tanzania, Winstone Odhiambo.
WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo ili kuwanusuru wananchi wake na njaa kampuni ya mbolea ya Yara imezindua bima ya mazoa ili kuwakinga wakulima dhidi ya hasara mbalimbali kwenye sekta hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bima hiyo leo Machi 28, 2023 Mkurugenzi wa Yara Tanzania Winstone Odhiambo amesema kuwa Yara kupitia mpango wake wa Africaconnect kupitia kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance.

"Kampuni ya Yara Tanzania, kupitia mpango wake wa Africaconnect, leo inazindua huduma mpya na kabambe ya kuwalinda wakulima wa Tanzania dhidi ya hasara ya kuharibika kwa mazao itokanayo na madhara ya mabadiliko ya tabianchi kama vile hali mbaya ya hewa" amesema Odhiambo.

Amesema kuwa awali mpango wa Africaconnect ilizinduliwa mwaka 2022 ambapo wakulima wa mpunga 83,000 waliojiunga na mpango huo wananufaika na huduma za kifedha, upatikanaji wa mbolea bora, huduma za ugani pamoja soko la uhakika kwa mazao yao.

“Hatua hii ni kubwa kwetu tunaposhughulika kuwawezesha wakulima kupata riziki yao na kulinda usalama wa chakula. Kwa kujiunga na Africaconnect, kampuni ya Jubilee Insurance imeongeza msukumo wa kufanya kilimoTanzania kuwa thabiti na chenye faida”amesema Odhiambo.

Mbali na Jubilee washirika wengine wa Africaconnect ni benki ya Equity, Corteva Agriscience, Wakala wa Taifa wa Uzalishaji na Uendeshaji Mbegu za Kilimo (Agriculture Seed Agency) na kampuni ya Murzah Wilmar Rice Miller Ltd.

Jubilee Insurance imekuwa mshirika mpya kabisa kujiunga na mpango huo unaotoa suluhisho la uhakika katika kuongeza tija kwa wakulima.

Odhiambo amesema kuwa wakulima wanaopenda kujiunga na mpango huo wafike kwa mawakala wa mbolea wa Yara walio karibu nao, tawi lolote la Benki ya Equity au wapige simu bure kwenda namba 0800750188.

Kwa upande wake Dipankar Acharya Ofisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Jubilee Insurance , amesema kuwa mpango huo utawalinda na kuwanufaisha wakulima dhidi ya hasara ya mazao wanayoipata hasa katika kipindi hiki ambako kumekuwepo na mabadiriko ya tabia nchi.

“Tumefurahi kuwa washirika wa Africaconnect ili kuwalinda wakulima na hasara za mazao zinazosababishwa na majanga ya asili kwa kuwapa bima ya mazao na ushughulikiaji bora wa hatari wanazokabiliana nazo katika kilimo, kuwepo kwa mpango huu wa bima ya mazao, sasa tunatarajia wakulima watalima kwa matumaini makubwa.”

Kwa mafanikio dhahiri yaliyopatikana mwaka wa kwanza, mpango wa Africaconnect utatanua wigo wa huduma zake kwa wakulima wengi zaidi mwaka huu. “Hivyo tunayo furaha kutangaza leo kuwa mbali na wakulima wa mpunga, mwaka 2023 Africaconnect

Naye, mkurugenzi Mkuu wa Equity Bank, Isabela Maganga amesema kuwa Benki ya Equity kwa Mwaka 2022 ilitoa mikopo yenye thamani ya Sh. Bilioni 14 kwa wakulima 4600 wa mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Arusha, Manyara na Iringa kupitia mpango wa Africaconnect. Hadi asilimia 30 ya mikopo yote itolewayo na benki ya Equity huwalenga wakulima nchini.

"Wakulima watapata mikopo ya pembejeo isiyo na dhamana kutoka benki hiyo na tunatarajia kutoa huduma kwa wakulima wengi kutokana na ushirikiano wetu na Yara",amesema Maganga.

Meneja wa Yara Digital Solution kwa nchi ya Tanzania na Rwanda Deodath Mtei amesema kuwa Yara imeendelea kuwashika mikono wakulima kwa kuhakikisha kuwa wanazidi kupata ujuzi wa kulima kisasa ili wapate faida maradufu.

“Thamani wanayopata wakulima waliojiunga na Africaconnect ni pamoja na ujuzi wa kitaalamu, pembejeo za ubora wa juu na masoko ya uhakika. Tunaamini kwamba mkulima aliyewezeshwa ni mkulima mwenye ustawi,” amesema Mtei.

Upendo Daniel, mjane anayejishughulisha na kilimo cha mpunga wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro amesema kuwa kabla ya mpango huo alishindwa kupata mkopo lakini kupitia mpango wa Africaconnect ameweza kufanikiwa.

“Kwa kutumia shamba langu dogo ilikuwa haiwezekani kupata mkopo kwa kuwa taasisi za kifedha hazikuwa tayari kuniidhinisha...Naishukuru Yara kwa kutuletea Africaconnect na sasa naweza kuwalisha na kuwasomesha watoto wangu.”

Amesema, mwaka jana, alifanikiwa kuongeza uzalishaji katika shamba lake la robo eka na kutoka magunia manne hadi 11 ya kilo 100

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...