Dar es Salaam, Jumatano 12 Aprili 2023: Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na benki ya Letshego wametangaza washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde.

Akizungumza mara baada ya kutangaza washindi hao, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema kuwa promosheni hiyo itakuwa ya muda wa wiki nane na inalenga kuhuisha na kuhamasisha wateja wa Airtel Money na jamii kwa ujumla kujijenga utamaduni wa kuweka akiba kidigitali. Airtel Money tunajisikia Fahari sana tunapoendeleza ubunifu katika huduma hii ya Airtel Money inayokuwa kwa kasi huku wateja wakijihudumia kidigitali kupitia Airtel Money.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Hazina benki ya Letshego Esther Chamwene alisema kuwa promosheni ya Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde inawazadia wateja wote wa Airtel Money wanaoweka akiba kupitia Timiza akiba kuanzia wiki iliyopita ambapo hadi kufikia mwisho wa promoshen wateja 203 watakuwa wameibuka washindi wa promosheni hii. 

"Tutakuwa na droo moja kila wiki ambapo Wateja 25 watashijishindia sh 20,000 kila mmoja na tutawawekewa pesa zao za zawadi moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money, vilevile tutatoa zawadi ya bajaji mpya, pikipipiki mpya, pamoja na luninga mpya (flatscreen) kwenye droo ya mwisho ya promosheni hii", alisema.

Promosheni ya Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde ambayo inaendesha na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na benki ya Letshego ilizinduliwa wiki iliyopita na itatudumu kwa muda wa wiki nane huku ikiwa na lengo la kuhamasisha wateja wa Airtel Money na Watanzania kwa ujumla kuendelea kujiwekea utamanduni wa kujiwekea akiba huku wakijiwekea kwenye nafasi ya kushinda fedha taslimu au bajaji mpya, pikipipiki mpya, pamoja na luninga mpya (flatscreen) kwenye droo ya mwisho ya promosheni hii.

Kwenye droo hiyo ya kwanza, washindi 25 wametangazwa ambapo kila mmoja ameweza kujishindia fedha taslimu Tzs 20,000.

Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) akizunguma wakati wa  droo ya washindi wa promosheni ya ‘Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde’ ambapo washindi 25 wamejishindia zawadi ya fedha taslimu 20,000 kila mmoja. Promosheni ya ‘Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde’ inaendesha na Airtel kupitia huduma yake ya Airtel money Timiza Akiba kushirikiano na Benki ya Letshego Tanzania huku ikiwa na lengo la kuhamasisha wateja wa Airtel Money na Watanzania kwa ujumla kujiwekea utamanduni wa kujiwekea akiba kidigitali. Kulia ni Meneja Huduma za Airtel Money Hellen Lymo na kati kati ni mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Elibariki Sengasenga.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...