Benki ya Exim Tanzania imekabibidhi msaada wa chakula na mahitaji muhimu kwa kwa kaya maskini 19 visiwani Zanzibar sambamba na kuandaaa futari mahususi kwa wateja wa benki hiyo visiwani humo ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuwa karibu zaidi na wateja wake wenye imani ya Kiislam katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani .

Katika matukio hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki visiwani humo ilishuhudiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Bw Hamza Hassan Juma akiongoza zoezi la kukabidhi msaada wa chakula na mahitaji mengine kwa familia hizo 19 kupitia  Jumuiya ya Shauri Moyo Development  Foundation huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Massoud Ali Mohammed akiongoza hafla ya futari kwa ajili ya wateja wa benki hiyo visiwani humo.

Akizungumzia matukio hayo Mkuu wa  Idara wa Masoko na Mawasiliano Benki ya Exim Bw Stanley Kafu alisema yanalenga kuiweka karibu zaidi benki hiyo na wateja wake wenye imani ya dini ya Kiislamu visiwani humo ili kuonyesha mshikamano na umoja baina ya pande hizo mbili hususani kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

“Tumekuwa tukiheshimu sana Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na ukweli kwamba, ni kipindi ambacho mwanadamu anajiweka karibu na Muumba wake kupitia mfungo na kufanya maombi.’’

“Hata hivyo siku zote Benki ya Exim tumekuwa tukiamini kwamba mafanikio makubwa ambayo tunaendelea kuyapata si tu kwasababu ya weledi katika utoaji wa huduma zetu bali pia ni kwasababu ya namna benki hii inavyoshirikiana na jamii yake. Kipindi kama hiki cha mfungo mtukufu kwetu sisi ni moja ya wakati muafaka kwetu kurejesha shukrani zetu kwa wateja wetu kwa kuandaa matukio ya futari pamoja na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa na wenye uhitaji,’’ alisema.

Bw Stanley aliahidi ushirikiano zaidi baina ya benki hiyo na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuhakikisha uhusuano uliopo baina ya benki hiyo na wafanyabiashara pamoja na wadau wa sekta ya Utalii visiwani humo unaendelea kuboreshwa zaidi ili kuendelea kujenga uchumi wa visiwa hivyo.

Wakizungumza kwenye matukio hayo Waziri Hamza Hassan na Waziri Masoud Ali Mohammed pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa kuandaa matukio hayo waliahidi kwa niaba ya serikali ya SMZ kuendeleza ushirikiano na benki hiyo ili kuunga mkono adhima yake kuinua uchumi wa visiwa hivyo kupitia sekta ya biashara na utalii.

“Kwa matukio mliyoyafanya hii leo visiwani Zanzibar mnadhihirisha dhamira yenu njema ambayo si tu kuhudumia jamii hii ya Wazanzibar kupitia huduma zenu za kibenki bali pia kushirikiana nao hata kwenye masuala yanayohusu imani yao.’’

“Zaidi mmeamua kusaidia hata jamii ya watu wasiojiweza kiuchumi ambao wengine hata sio wateja wenu ila mmefanya yote haya kuhakikisha makundi yote yanafurahia Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani…tunashukuru sana na tunaahidi ushirikiano zaidi,’’ alisema Bw Masoud Ali Mohammed wakati akitoa nasaha zake kwenye hafla hiyo fupi ya futari.

Hafla hiyo ya futari ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Bw Hamza Hassan Juma (wa pili kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa chakula na mahitaji muhimu kwa mmoja wa wananchi wenye uhitaji visiwani humo uliotolewa na Benki ya Exim Tanzania ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuwa karibu zaidi na wateja wake katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Pamoja nae ni Mkuu wa  Idara wa Masoko na Mawasiliano Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (katikati) pamoja na maofisa wengine waandamizi wa benki hiyo visiwani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Massoud Ali Mohammed (wa kwanza kulia) sambamba akiongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Bw Hamza Hassan Juma (wa kwanza kulia) wakiwaongoza wageni wengine waalikwa kupata chakula wakati hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wateja wake visiwani humo. Hafla hiyo ya futari ilifanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Bw Hamza Hassan Juma (kushoto) akionesha sehemu ya msaada wa chakula na mahitaji muhimu kwa mmoja wa wananchi wenye uhitaji visiwani humo uliotolewa na Benki ya Exim Tanzania ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuwa karibu zaidi na wateja wake katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Pamoja nae ni Meneja Mahusiano Msaidizi Benki ya Exim tawi la Zanzibar Bw Aziz Khamis (kulia)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Bw Hamza Hassan Juma (alievaa kanzu na koti) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya Exim,  viongozi wa Jumuiya ya Shauri Moyo Development  Foundation pamoja na wanufaika wa  msaada wa chakula na mahitaji muhimu uliotolewa na Benki ya Exim Tanzania ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuwa karibu zaidi na wateja wake katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Massoud Ali Mohammed (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wateja wake visiwani humo. Hafla hiyo ya futari ilifanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Mkuu wa  Idara wa Masoko na Mawasiliano Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ya futari ilifanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Massoud Ali Mohammed (katikati) akibadilishana mawazo na wageni wengine waalikwa akiwemo Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Simai Mohammed Said (Kushoto) pamoja na Mkuu wa  Idara wa Masoko na Mawasiliano Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (kulia) wakati hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wateja wake visiwani humo. Hafla hiyo ya futari ilifanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Massoud Ali Mohammed (wa sita kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Bw Hamza Hassan Juma (katikati) na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Simai Mohammed Said ( wa sita kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya Exim Tanzania wakati hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani humo. Hafla hiyo ya futari ilifanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Sehemu ya wageni waalikwa wakipata futari wakati wa hafla hiyo.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...