Na Said Mwishehe, Michuzi TV - Uwanja wa Mkapa

LICHA ya mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam,mashabiki wa soka la Tanzania wameendelea kujitokeza kwa wingi katika dimba la Benjamin Mkapa kwa ajili ya kushuhudia mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga.

Mtanange huo unatarajia kuanza saa 11 jioni na tayari mashabiki wameshakaa kwenye viti kusubiri kuona wanaume 22 ambavyo wataonesha misuli baada ya kusubiri mchezo huo kusubiriwa kwa hamu kubwa huku mashabiki wa pande zote mbili kila mmoja akiamini kuibuka na ushindi.

Hata hivyo hadi saa 9:15 alasiri mashabiki wa Simba wameonekana kuwa wengi ukilinganisha na mashabiki wa bingwa mtetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara lakini muda bado upo na uwezakano kwa mashabiki wa timu zote kuujaza uwanja ni mkubwa.

Tambo ndani ya uwanja zinaendelea huku Yanga wakiamini Simba hana ubavu wa kuifunga Yanga ambayo chini ya Kocha Profesa Nabi imeimarika na kuwa tishio ukijulimsha na mashuti ya mshambuliaji wao Aziz Ki ndio hatari kabisa .

Nje ya uwanja wa Mkapa misusuru mikubwa ya mshabiki imejipanga kwa ajili ya kuingia uwanjani huku burudani mbalimbali za vigoma vikichukua nafasi , mashabiki wamepagawa kabla ya mchezo .Kama unavyojua tena muziki wa singeli nao hauko nyuma, mispika mikubwa inaendelea kutumbuiza tu, yaani raha bin raha.

Wakati mchezo huo ukitarajiwa kuanza mida hiyo ya saa 11 jioni , Yanga imekuwa na rekodi nzuri kwa miaka ya hivi karibuni ambapo imekuwa ikiibuka na ushindi lakini wakati huo huo mashabiki wa Simba nao wanaamini mchezo wa leo wanakwenda kuondoa uteja

Kwa upande wa machoka na wachezaji wa timu mbili wameeleza kuhusu mchezo huo na kila mmoja akijinasibu kuibuka na ushindi kutokana na maandalizi ambayo yamefanyika kuelekea mchezo huo ambao ni miongoni mwa michezo inayofuatiliwa na mashabiki wengi wa Soka Afrika Mashariki na Kati na hiyo inatokana na ubora wa timu hizo na wingi wa mashabiki wake.

Pamoja na yote ni ngumu kutabiri nani ataibuka na ushindi, hivyo dakika 90 za mchezo zitaamua nani atapeleka kilio kati ya Simba au Yanga.Michuzi TV iko uwanjani kwa Mkapa kuhakikisha msomaji wake hakuna kinachokupita.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...