TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), watembelewa na ujumbe kutoka Chama cha elimu cha Kimataifa cha China (China Education Association of International Exchange (CEAIE) kwaajili ya kuendeleza ushirikiano wao na Taasisi ya Chongqing Vocation Institute of Engineering (CQVIE).

Kaimu Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Najat Mohammed akizungumza wakati wa mazungumzo na ujumbe huo jijini Dar es Salaam Aprili 03, 2023. Amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na taasisi za kimataifa ili kukuza ubora wa elimu kupitia kutafuta na badilishana uzoefu pamoja na nyenzo za kujifunzia.

Amesema kuwa DIT wanaunga mkono juhudi za taifa na kikanda kwa kutoa mafundi waliobobea na wanaohitajika katika soko la ajira.

Prof.Najat amesema ili kufanikisha hilo tunatakiwa kuhakikisha tunakuwa na miundombinu, nyezo za kufundishia na kuwajengea uwezo wafundishaji ili kuwa na wataalamu wengi Zaidi.

Aidha DIT imekuw ikitoa mafunzo ya vitendo kwa kuwapeleka wanafunzi katika viwanda mbalimbali hapa nchini ili kupata ujuzi kulingana ujuzi unaohitajika katika maeneo ya kazi.
Makamu wa Rais wa Chama cha elimu cha Kimataifa cha China (China Education Association of International Exchange (CEAIE), Liu Limin   akizungumza wakati walipotembelea Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) jijini Dar es Salaam Aprili 03, 2023.
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Najat Mohammed akizungumza wakati walipotembelewa na ujumbe kutoka Chama cha elimu ya China jijini Dar es Salaam Aprili 03, 2023.
Dkt. Noeli Mbonde wa Kwanza kulia akizungumza kwa niamba ya Mwakilishi wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda jijini Dar es Salaam Aprili 03, 2023 wakati ujumbe wa Chama cha elimu cha Kimataifa cha China (China Education Association of International Exchange (CEAIE).
Wang Yongli wa pili kulia akizungumza wakati walipotembelea Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) jijini Dar es Salaam Aprili 03, 2023.



Matukio mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...