Mtuhumiwa huyo inadaiwa alikuwa kiongozi wa kikundi cha mtandaoni kwenye jukwaa la "Discord" ambapo nyaraka za siri za Pentagon zilidownload, na kwamba ndiye aliyedhibiti seva ya kikundi hicho, kilichoitwa "Thug Shaker Central" chenye kujumuisha watu kati ya 20 na 30, wanaume na vijana, ambao walishirikiana katika kupenda bunduki, katuni za ubaguzi wa rangi na michezo ya video.
Teixeira ni askari wa kikosi cha wanajeshi wa anga wa Massachusetts Air National Guard, ambaye alihamia kituo cha ndege cha Andrews Air Force Base hivi karibuni na hivi karibuni alibadilisha nambari yake, mama wa mpiganaji huyo wa anga aliiambia New York Times.
Hata hivyo, haijajulikana mara moja endapo Teixeira alikuwa na uwezo wa kufikia nyaraka hizo za juu kabisa za siri na nyingine. Lakini inasemekana kwamba nyaraka hizo kwa kawaida huwasili kwa njia ya barua, ambazo zinaweza kuhamishiwa kwa watu wengine.
Wanachama wa kikundi chake cha mtandaoni walidai kwamba nyaraka hizo zilichapishwa toka miezi kadhaa iliyopita, kwa madhumuni ya habari tu na hawakupaswa kuondoka nazo nje ya grupu.
Pentagon ni makao makuu ya Idara ya Ulinzi ya Marekani na ipo Arlington, Virginia, karibu na Mto Potomac sio mbali sana kutoka Washington, D.C. Ni moja ya majengo makubwa ya ofisi duniani, lenye eneo la sakafu la takriban futi za mraba milioni 6.5 na wafanyakazi zaidi ya 23,000.
Pentagon ilikamilika mwaka 1943 na hutumika kama kitovu cha misheni ya kijeshi ya Marekani, na Waziri wa Ulinzi na maafisa wengine wa ngazi za juu ya kijeshi hufanya kazi kutoka ofisi zake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...