Msanii mwandamizi kwa kipaji na na kusomea.
Kuelekea mwishoni mwa miaka ya sabini mkoani Iringa Mgunga (wakati huo akiitwa Emanueli) pale mjini Iringa hakukosekana katika uwanja wa michezo wa Samora ambapo maadhimisho ya kitaifa yalifanyika na sanaa za maonyesho na muziki vilitia nakshi matukio hayo.
Mvuto mkubwa kwa mgunga ulikuwa kwa shule tatu za msingi ambazo kila sherehe zilikuwa kivutio kikubwa kutokana na umahiri wao katika sanaa za kuimba,kuigiza, ngonjera na ngoma. Kati ya shule hizi kikundi kimoja kiliongozwa na mwalimu mahiri John Komba ambaye baadaye alikuja kuwa msanii mkubwa wa kitaifa akiwa Kapten John Komba. Cheche za kupenda sanaa zilianzia hapo.
Mhula wa sekondari ,Mgunga alikuwa katika shule ya sekondari Mawenzi Mjini Moshi. Hii ni shule iliyokuwa na msisimko mkubwa wa kisanii kwani ulikuwa na mashindano ya sanaa za maonesho na muziki kila mwaka. Shule iligawanywa katika makundi manne na kuitwa “Nyumba” nazo zilikuwa MAWENZI, KIBO, MERU NA ASHIRA. Mgunga akiwa kidato cha pili; kwanza akachaguliwa kwa kura kuwa mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM wa shule na pili akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa Nyumba ya MAWENZI.

Yote haya yalitokana na ushiriki wake katika sanaa ambao pia ulileta ushindi mkubwa katika nyumba yake. Miaka minne ya Mawenzi ilimtambulisha Mgunga kama Mtunzi maarufu na mtendaji wa maigizo, Mashairi na Ngonjera. Yeye na mwananfunzi mwenzake aliyeitwa Zaina Bongi ambaye baada ye alikuja kuwa mtangazaji wa Redio Tanzania na TBC waliwika sana katika uoneshaji wa ngonjera. Hii ilimpa fursa ya kushiriki katika mashindano mbalimbali ya sanaa ya kitaifa .
Mgunga alifanya maamuzi mapema sana kuhusu taaluma ya kusomea. Akiwa kidato cha pili aliamua kwamba ama angekuwa Mwanasanaa ama Mwaana habari! Kwa kusingatia chaguo hilo Mgunga aliwekeza bidii kubwa katika masomo ya Kiswahili, kifaransa na Kiingereza. Alisoma sana maudhui yaliyohusiana na harakati za ukombozi wa Afrika, historia,utamaduni na fasihi.
Kutokana na hisia za kisiasa na umajumuia wa kiafrika Mgunga na mwananfunzi mwenzake Maiko Mlingi wakiwa wanafunzi pekee waliungana na watembea kwa miguu zaidi ya miamoja kutoka kanda ya Kaskazini kuelekea Dodoma kutokea Arusha Ikiwa ni maadhimisho ya miaka 20 ya Azimio la Arusha
Alifaulu na kuchaguliwa Kwenda sekondari ya Milambo kwa masomo ya Kiswalihi,Fasihii kwa Kiingereza na Kifaransa (KLF). Kutokana na matatizo ya kiafya baada ya miezi miwili yeye na mwenzake walihamia shule ya sekondari ya wasichana ya ZANAKI ya jijini Dar es alaam hivyo kuwa wavulana wa kwanza kusoma katika shule ya wasichana,.
Moto wa sanaa ni kama ulitiwa petroli kwani Mgunga kwa kasi alitunga na kuongoza kazi mbalimbali za sanaa shuleni Zanaki zikiwemo LINAUBANI tamthiliya ilioandikwa na Penina Mhando.Mgunga pia aliendeleza utamaduni wa kuangalia maonesho ya vikundi vya sanaa jijini mathalani Muungano, Mandela, Bora, Relwe, Makutano nk.
Baada ya kumaliza kidato cha sita Mgunga alijiunga na Jeshi lakujenga Taifa kwa mujibu wa sheria kambi ya Makutupora Dodoma. Huko nako alichaguliwa katika kikundi cha sanaa cha kikosi na kupewa wadhifa wa Uenyekiti. Katika kikundi alikutana na wasanii wahitimu wa chuo cha sanaa cha Bagamoyo ambao pia walimtia hamasa kuipenda fani ya sanaa.

Kipindi cha mwaka mmoja kutumikia JKT Mgunga pia alisaidia kikundi kushinda mashindano mbalimbali ya kimkoa na kitaifa ambapo kikundi kiliwakilisha mkoa katika mashindano ya kanda Tabora na Kitaifa moani Morogoro.
Mwaka 1991 Mgunga aliombwa na uongozi wa kikundi cha sanaa cha Nyota kilichokuwa chini ya Makao Makuu ya CCM Dodoma kama mwalimu na mmoja wa viongozi wake.Alisaidia kikundi hicho kiufundi mpaka alipoondoka mwaka 1992 kujiunga na chuo kikuu cha Dar es alaam kwa masomo ya Sanaa za Maonesho na Ualimu.
Mwaka 1994 Mgunga alianzisha kikundi cha sanaa cha Parapanda Arts ,baadaye kikaaitwa Parapanda Theatre Lab. Huku akiwa mwanafunzi Mgunga aliandaa maonesho kadhaa na kufanywa ndani na nje ya chuo ili kuimarisha ujuzi kivitendo. Mwaka 1996 alihitimu na kuendelea na kikundi huku makao yake yakihamia Mabibo .
Mgunga aliliongoza kundi la sanaa kwa umahiri ,ubunifu na kujitoa sana hata kufanya moja ya kundi bora la sanaa za maonesho Tanzania na Afrika Mashariki.Mgunga aliasisi mtindo wa sanaa za maonesho ambayo haukukumbatia uigizaji tu bali zaidi usimulizi,utambaji, uigizaji,na uchezaji (Narrative Theatre) mtindo uliokipa kikundi umaarufu sana nje ya nchi ambako mtindo wa kimagharibi ulikuwa umeshika hatamu.
Miaka ya elfu mbili Mgunga alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es alaam kwa masomo ya shahada ya uzamili katika Sanaa za Maonesho na Chuo kikuu cha Muhimbili katika shahada ya uzamiri katiaka Sayansi ya Mabadiliko ya Tabia.
Miongoni mwa maonesho makubwa aliyotunga ama kuandaa ni Pamoja na SAMAKI WA DHAHABU, MFALME SALTANI NA MWANAE GUIDONI, BONGO DAR ES ALAAM, NGUZO MAMA(ya Penina Mlama), MKWEZI NA MNAZI,WIMBO WA NYONGA, WIMBO WA JANDO , SAUTI KUTOKA MAZIMBU, na ANTIGONE onesho lililoandaliwa nchini Uswidi na kuonyeshwa huko na Tanzania.
Baadhi ya nchi alizotembelea kwa warsha na maonesho ni Kenya,Uganda, Rwanda, Zambia, Afrika Kusini, Urusi, Marekani, Uingereza,Ujerumani ,Ufaransa na Ethiopia
Mgunga Muwezeshaji na mwalimu
Kwa zaidi ya miaka 25 Mgunga amekuwa mwalimu wa wasanii wengi na vikundi vya sanaa hasa katika fani za Sanaa kama Methodolojia ya mawasiliano,uponyaji na ufundishaji darasani. Kutoaka na ujuzi katika mbinu za Mawasiliano yenye kubadili tabia(Social Behavioral Change Communication-SBCC) Mgunga amekuwa mtaalamu elekezi kwa taasisi nyingi zinazotumia sanaa kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Ameshiriki katika miradi mingi ya afya, uongozi na utawala, ulinzi na uwezeshaji watoto na vijana. Baadhi ya mashirika na taasisi ni UNICEF, SAVE THE CHILDREN, PLAN INTERNATIONAL, JHPIEGO,nkAidha amefanya kazi na asasi za serikali zikiwemo wizara za Elimu, Afya na Mendeleo ya jamii.
Mgunga na Babawatoto Organization
Baada ya kuiongoza taasisi ya parapanda kwa miaka 17 ,mwaka 2011 Mgunga aling’atuka na kushika hatabu katika asasi ya kiraia aliyoshiriki kuanzisha mwaka 2006 ikiitwa Babawatoto. Hii ilikuwa ni hatua nyingine ya kuendelea kufanya kazi na watoto na vijana wadogo jambo alilo na mapenzi nalo sana. Babawatoto ilitoa fursa ya kufanya kazi na watoto na vijana wengi zaidi na pia kutoa uwanja mpana wa kutumia sanaa kama mbinu lakini pia kama kazi kwa kuwafunza vijana wengi walio katika mazingira magumu ili wajiajiri kupitia sanaa.
Nifuraha kwamba viajana zaidi ya 400 wamepitia katia taasisi ya Babawatoto ambayo ina ktuo cha watoto na vijana pale Mburahati. Sehemu kubwa ya vijana wanaofanya sarakasi hasa Dar es alaam wametokea Babawatoto. Hivi sasa vijana wengi wako katika makampuni makubwa ya sarakasi ulaya ,Uchina na Uturuki. Kwa Tanzania vijana hawa wengi wao wana mikataba na Mama Afrika na Mrisho Mpoto ambaye ni mmoja kati ya waliofunzwa na Mgunga.
Babawatoto inafanya kazi kwa watoto walio katika mazingira magumu hasa wa Mitaani kwa jiji la Dar es alaam na katika kambi za wakimbizi Mkoani Kigoma kuanzia mwaka 2015.
Mgunga kwa sasa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Babawatoto Organization and Mkurugenzi Mwanza wa Chimbuko Arts Media Limited kampuni ya kuendeleza sanaa nchini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...