Maafisa Utamaduni wa Wilaya za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wamepatiwa mafunzo ya kuimarisha Utendaji wao katika kukuza Sekta ya Utamaduni katika maeneo yao ya kazi.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tatu kuanzia Aprili 14 hadi 16 Mjini Bagamoyo na yatahusisha mada mbalimbali chini ya Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt. Emmanuel Temu.
Miongoni mwa mada zilizowasilishwa kwa siku ya Aprili 14, 2023 ni pamoja na Majukumu ya Maafisa Utamaduni Kisera na Kimundo, Uhifadhi na Uendelezaji wa Urithi wa Utamaduni pamoja na Uhifadhi na Uendelezaji wa Urithi wa Bara la Afrika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...