Katibu wa kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis amesema chama cha mapinduzi CCM zanzibar kitaendelea kuthamini mchango wa wazee kutokana na kujitoa muhanga kwa ajili ya kuikomboa nchi.

Mbeto amesema hayo wakiti akikabidhi sadaka ya fedha taslimu kwa wazee wa baraza la wazee wa chama cha mapinduzi ofisi kuu CCM Zanzibar amesema kitendo cha wazee kujitolea kwa ajili ya kufanya mapinduzi ya mwaka 64 ni kikubwa na kitaendelea kukumbukwa na kuthaminiwa siku hadi siku.

Amesema historia inaonyesha kuwa mchango wa wazee katika nchi hii hautasahaulika kutokana na maendeleo makubwa waliyoyanzisha hivyo chama chama cha mapinduzi kitaendelea kuwaenzi wazee na kuchota hekima na busara zao ili nchi izidi kupiga hatua zaidi kimaendeo.

" katika maandiko matakatifu ya Vitabu vya dini vimemtaja mzee kuwa hana cha kulipwa hivyo mungu amempa darja kubwa mzee alisema mbeto"

Amefahamisha kuwa kutokana na darja kubwa waliyopewa wazee CCM itahakikisha inawawekea mazingira mazuri wazee ili kufaidika na matunda ya nguvu zao walizozitoa wakati wanaikomboa nchi.

"Wamefanya mapinduzi bila ya kutumia mizinga wala silaya yoyote wametumia nguvu zao na kuikomboa serikali ambayo vijana wa leo wanaiyongoza alisema mbeto"

Aidha Mbeto amewaomba wazee hao waendelee kuwalea na kuwashauri iwapo wanapoona kunajambo haliendi sawa katika kukitumikia chama ili kuhakikisha viongozi wanafanya kazi vizuri za utekelezaji wa ilani.

Akitoa neno la shukran kwa niaba ya wazee wenziwe wa baraA la wazee wa wa chama cha mapinduzi ofisi kuu Zanzibar mzee Talib Mussa Makungu ameishauri chama cha mapinduzi kwa kuwajali na kuwathamini wazee huku akimuhakikishia mwenezi kuwa wataendelea kukitumikia chama muda wote wanapohitajika ili chama kizidi kuimarika

Katibu wa kamati Maalum ya NEC,Idarea ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis amekamilisha ziara yake ya kukutana na wazee wa baraza la wazee wa chama cha mapinduzi ofisi kuu Zanzibar ambapo ziara kama hiyo anatarajia kuifanya kisiwani pemba.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...