Na Byarugaba Innocent,Kibaha.
SHULE ya Sekondari Viziwaziwa inayojengwa Kata ya Viziwaziwa Halmashauri ya Mji Kibaha kupitia Secondary Education Quality Improvement Project (SEQUIP) umefia 97% ya ujenzi huku kazi ndogondogo zikiendelea kufikia 100% huku jumla ya Shilingi 540,000,000 zikitumika.

Tayari miundombinu yote ikiwemo Madarasa 8,Maabara 3 za sayansi,maktaba,chumba cha TEHAMA,Jengo la utawala,matundu ya vyoo 20 pamoja na miundombinu ya Maji imeshafikia Kiwango cha kuwaruhusu wanafunzi 230 kuanza masomo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa awali fedha iliyoidhinishwa na Serikali ni Shilingi 470,000,000 hata hivyo Halmashauri iliongeza milioni 70,000,000 kutokana na kupanda kwa gharama za ujenzi ili kukamilisha miundombinu yote ya Shule hiyo itakayokuwa na kidato cha 1-6

Kaimu mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Edward Jidamva ameeleza kuwa shule imesajiliwa kwa namba S.6158 huku wanafunzi 230 waliokuwa wakitembea zaidi ya kilomota 15 kuifuata shule ya Sekondari Miembesaba wakiwa wanufaikaji wa mwanzo

Diwani wa Kata ya Viziwaziwa Mhe.Mohamedi Chamba amesema kitendo cha Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kujenga shule hiyo ni mwendelezo wake wa kuitekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 kuhakikisha kila kata inapata shule ya Sekondari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...