Na Victor Masangu,Kibaha
MKE wa mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Selina Koka ameahidi kuwainua kiuchumi wanawake wa kata ya misugusugu na kongowe kwa kuwawezesha kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali pamoja na kuwapatia mitaji ya fedha ili kuondokana na umasikini.

Selina ambaye pia ni mlezi wa UWT Wilaya ya Kibaha mji amesema lengo lake kubwa kuwapambania wanawake wote was uwt kwenye Jimbo la Kibaha kwa kuwasaidia waweze kufanikiwa katika shuguli zao mbali mbali za ujasiriamali.

"Ninachotaka kukifanya ni kuwawezesha wanawake wajasiriamali ili waweze kuanzisha biashara zao ambazo zitawasaidia kujipatia fedha na kujikwamua kiuchumi na kwamba nitasaidia katika kata zote 14 za Jimbo hili,"alisema Mgonja.

Alifafanua zaidi Selina Koka aliongeza kuwa mikakati yake ni kuwafungulia akaunti wanawake wa UWT kwa kuwapa kiasi cha shilingi laki tano ili waweze kuanzisha biashara.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mji Elina Mgonja amebainisha kwa kwa sasa katika kata ya misugusugu kumekuwa na maendeleo katika sekta mbali mbali.

Aliongeza kuwa Mbunge Koka amekuwa mstari wa mbele katika kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakali na kuzifanyia kazi katika maeneo ya afya,elimu pamoja na miundombinu ya barabara.

"Kitu kitubwa sisi wanawake inabidi tuachane kabisa na mambo ya makando kando na kuwahimiza watu kulipa ada kwa wakati lengo ikiwa ni kujizatiti katika kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,"alisema Mgonja.

Katika hatua nyingine alimpongeza kwa dhati mlezi wa UWT Selina Mgonja kwa juhudi zake za kusaidia wanawake katika kuwawezesha ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kwamba ziara yake ni kuangalia uhai wa chama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...