Na Mary Margwe, Naisinyai-Simanjiro.

Mkurugenzi mzawa wa Kampuni ya Franone Mining Gems Ltd na Mmiliki wa Mgodi wa Kitalu C Onesmo Anderson Mbise ameahidi kutoa sh.mil.38 ili kuisaidia kutatua baadhi ya changamoto inayoikabili shule ya Sekondari ya kidato cha sita Naisinyai iliyopo Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Mbise ambaye alikua Mgeni rasmi kwenye mahafali ya kwanza ya kidato cha sita katika shule hiyo, amesema yeye ni Mwekezaji mzawa na sio Mgeni kama ambavyo wanajua baadhi ya watu, hivyo atahakikisha changamoto kubwa kubwa wanazimaliza katika shule hiyo.

Alisema sera ya Serikali inasema " Kama tumewekeza Mahali ni lazima kurudisha kile kidogo unachopata Kwa jamii inayokuzunguka , hivyo sisi ni Watanzania na tunasaidia jamii maeneo mbalimbali yanayotuzunguka .

Aidha alisema miongoni mwa changamoto alizoahidi kutatua kuwa ni pamoja na jiko la kudumu la shule, ambapo wanafunzi wanahatariaha afya zao kutokana na wimbo kubwa la vumbi linalokipitia chakula chao, kutokana na hali ya kijiografia, ambapo hilo ameahidi kulichukua na kutatua changamoto hiyo (Haina bajeti yake)

" Changamoto nyingine ni mnaomba kisima Cha maji kilichaanzishw siku nyingi kiweze kukamilika ili kiweze kutoa kutoa huduma ya maji,ambacho kinahitaji Mtandao wa mabomba ya solar, hii mmeniambia inakadiliwa kutumia sh.mil.18, hili nalo ni muhimu sana nalichukua nnitalifikiaha kwenye Kampuni yangu, nitakaa na bodi kuweza kutatua hii changamoto muhimu" alisema Mkurugenzi Mbise.

Changamoto zingine ni umaliziaji wa vyumba vya Walimu ( Two in One ) ambayo Iko kwenye hatua ya umaliziaji ambao unakadiliwa kugharimu jumla ya sh.mil.20, umeme kwenye bweli la wasichana ( gharama yake haijawekwa ) vyote hivyo ameahidi kutatua changamoto hizo.

Awali Mbise alisema Shule ya Sekondari ya Naisinyai ni miongoni mwa ni miongoni mwa shule za mwanzo za kata zilizoanza 2006, ambapo aliipongeza Serikali kwa kuweza kujenga shule za kata ambazo zimeokoa watoto wengi wakiwemo wa jamii Cha kifugani hususania wasichana.

"Awali kabla ya kuwa na shule za Kata wanafunzi walio wengi wakihitimu Darasa la Saba walikua wanaenda kuolewa, ama kufanya kazi za nyumbani kama za kuchunga mifugo, lakini hapa Leo tumeona kuna binti aitwaye Maria amekuja hapa anaimba vizuri kabisa, hapa tunaona sasa umuhimu mkubwa wa kuwa na shule za kata, hivyo Serikali iliona mbali sana, hivyo ni vema tukaipongeza Serikali kwa jinsi ilivyokua imepata hilo wazo la kuanzisha shule hizo za kata" alisema Mbise.

Aidha alisema Shule hiyo ilianzia kidato cha 1-4 ,ambapo baadaye Serikali iliona ni vema sasa ikawa na kidato cha 5-6 kutokana na kuona ina Maendeleo mazuri " Nimesikia kuwa kidato cha 5-6 wanaotoka sehemu mbalimbali ndani ya Tanzania kama Mwanza, Kigoma, Arusha, Kagera, MManyara yenyewe na kwingineko, hata matokeo ya kidato cha nne Mkuu wa Wilaya yetu ya Simanjiro ameninon'goneza kuwa Shule hii inafanya vizuri sana.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo hakusita kuwaasa wahitimu hao kuepuka makundi yasiyo na maadili memamkwa jamii ili kuendelea kuilinda nidhamu, hekima waliofundiahwa wakiwa shuleni, Kwa kufanya hivyo kutawasaidia kuepuka ana makundi maovu" Na niwaambie huko mnakoenda majumbani hakuna sio kugumu na wala sio kurahisi msije makajiingiza kwenye makundi au kwenye mikumbo isiyosahihi kwenu, inategemea nyie wenyewe mnalichukuliaje, Yale mliyofundishwa shuleni yashikeni sana kwani yatawasaidia, kufuata mikumbo haitawasaidia chochote" aliongeza Mbise.

" Angalieni kila mtu anaangalia maisha yake, hata sisi tumepitia huko lakini sio kwenye mabaya, lakini leo mmeona nimeweza kusimama hapa mbele yenu kuzungumzia Maendeleo nya shule na namna ya kuwasaidieni, na nyie pia msituangushe Kuna siku mnaweza kualikwa kama Mimi nilivyoakikwa kuwa Mgeni wenu rasmi katika mahafaliyetu ya kwanza ya kidato cha sita,lakini mkiemda huko mkipotea tutakua tumepotezaTaifa letu la kesho" alisisitiza Mkurugenzi wa Kampuni ya Franone Mining Onesmo Anderson Mbise.

Hata hivyo ikumbukwe kuwa Serikali ilitangaza tenda Aprili mwaka 2022, ambapo kampuni ya Franone Mining Gems Ltd ilishinda tenda hiyo na mwezi wa sita na ilipewa leseni ya uchimbaji mwezi wa saba mwishoni huku serikali ikiwa na ubia wa asilimia 16 na mpaka sasa umeanza kazi za uchimbaji ikitegemea kuanza uzalishaji wa madini ya Tanzanite wakati wowote kuanzia sasa.

👇👇👇👇👇👇👇

Matukio mbalimbali ya mahafali ya kwanza ya kidato cha sita Naisinyai


Mwenye shati la drafti ni Mkurugenzi mzawa wa Kampuni ya Franone Mining Gems Ltd na Mmiliki wa Mgodi wa Kitalu C Onesmo Anderson Mbise ameahidi kutoa sh.mil.38 ili kuisaidia kutatua baadhi ya changamoto inayoikabili shule ya Sekondari ya kidato cha sita Naisinyai iliyopo Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Picha na Mary Margwe.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...