Na Jane Edward, Arusha
Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari ya matumizi ya plastic na uchomaji wa taka za plastic ili kuepuka madhara mbalimbali ya kiafya yatokanayo na kemikali zilizotumika katika utengenezaji wa bidhaa hizo ikiwemo kuathiri mfumo wa tendo la ndoa kwa wanaume.
Hayo yameelezwa na Meneja baraza la usimamizi wa mazingira NEMC kanda ya kaskazini Lewis Nzali katika mkutano wa kukuza uelewa juu ya matakwa ya kanuni za usimamizi wa Mazingira na kupiga marufuku mifuko ya plastiki ya mwaka 2022.
Amesema kwa sasa serikali inajiwekeza katika kuona wananchi wake wakitunza mazingira lakini pia kuona afya za wananchi zikiimarika kwani plastiki iko kila mahali sio kwenye mifuko tu masokoni hata vikombe vya plastic nyumbani ni hatari.
"Kadri watumiaji wanavyoendelea kutumia plastic ndivyo ambavyo wanaendelea kujaza sumu kwenye miili yao ambapo baadae inaleta madhara kiafya kwahyo matumizi ya plastiki yanatakiwa kuachwa mara moja"Alisema Nzali
Licha ya kuwepo kwa vigezo na sifa za bidhaa zitokanazo na plastic zilizoruhusiwa kutumiwa kutokana na umuhimu wake, Bado vimeendelea kuwepo vilivyokosa sifa.
Afisa mdhiti ubora TBS kanda ya kaskazini Gabriel Bayo anasema vigezo na sifa ambazo mifuko mbadala iliyoruhusiwa kutumia inapaswa kuwa nembo ya ubora ya TBS ili kuweza kutumika katika shughuli mbalimbali.
Baadhi ya Viongozi wa masoko walioshiriki mafunzo hayo Jeremiah Katemi Mkuu wa soko la kilombero anasema mafunzo hayo yamekuwa msaada mkubwa kwao na wanaahidi kuwa mabalozi na kusimamia kutokuwepo kwa matumizi ya mifuko ya plastiki iliyokatazwa.
Ikumbukwe kwamba Mwaka 2019 Sheria ya kuzuia matumizi ya mifuko ya plastic ilipitishwa kwa lengo la wadau na wanachi kutoendelea kufanya matumizi ya plastiki yaliyokatazwa ambayo kiafya sio rafiki wa binadamu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...