Pamela Mollel,Arusha

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa hakutakuwepo na muda wa nyongeza katika utekelezaji wa miradi nane ya REGROW yenye thamani ya sh, bilioni 157.2.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba nane ya ujenzi wa majengo ya utalii,ujenzi wa viwanja vya ndege aliisisitiza hatasita kuwachukuliwa hatua wakandarasi watakao zembea kumaliza kazi kwa wakati sahihi kwa kuwa miradi hiyo imechelewa sana kufanyikana kwa zaidi ya miaka minne sasa

Alisema viwanja sita vya ndege vitajegwa ikiwemo Hifadhi za Ruaha viwanja vitatu, Hifadhi ya Mwalimu Nyerere viwanja viwili na Hifadhi ya Mikumi kiwanja kimoja

Waziri aliongeza kuwa katika hifadhi ya Udzungwa itajengwa njia ya juu ya utalii ya kilomita moja ambayo itakuwa njia ndefu katika njia zote Kusini mwa Afrika au Katika Nchi zaAfrika Mashariki.

Alitoa rai kwa wakazi wa mikoa ya kusini kuchangamkia fursa hivyo ya ujenzi wa miradi hiyo ili waweze kujipatia kipato

Aidha aliwataka Shirika la hifadhi za Taifa Tanapa kukuza utalii Kusini mwa Tanzania ili watanzania waone thamani ya miradi mbalimbali inayotekelezwa hapa nchini

"Acheni ukiritimba lazima tubadilike miradi huu uulikuwa ufanyike mwaka 2019 mnapita huku mnaingia huku sasa hii si faida kwa nchi yetu, simamieni mikataba acheni ukiritimba katika utekelezaji wa miradi mbalimbali haiwezekani Rais Samia Hassan Suluhu aseme ameleta miradi Kusini halafu watu wanakwamisha hapa lazima tuhakikishe mambo yaliyokwama yanafanya kazi ndio maana tunakwamua mambo mbalimbali yaliyokwama "

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dk, Hassan Abbas alisisitiza milango ya kufungua fursa za utalii Mikoa ya Kusini ifunguliwe ikiwemo kusaini mikataba hiyo nane kwaajili ya uboreshaji wa miundimbinu lengo ni kufungua fursa za utalii.

Alitoa onyo kali kwa maofisa manunuzi watakaokwamisha zoezi hilo kwa manufaa yao binafsi ili tu kukwamisha miradi hiyo kuwa atafute pa kwenda maana lengo la miradi ni kukamilika kwa wakati ili wafadhiri ambao ni Benki ya dunia watoe mkopo mwingine.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...