Mbunifu Majenzi (Arch) Robert Kintu wa NHC (aliyenyoosha kidole) akimwelekeza jambo Injinia Mburuga Matamwe (mwenye shati la dtaft) na Godfrey Mkumbo (kushoto) na Mhandisi Masumbuko Majaliwa, wakiangalia ramani ya maduka hayo.
Mbunifu Majenzi, Robert Kintu kutoka Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) akiangalia mchoro na Wataalamu Wengine.
Na Mwandishi Wetu, Kahama
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi kwa Mkandarasi wa Shirika eneo kunatakapoaza kujengwa majengo ya kitega uchumi yakiwamo maduka, supermarkets, maeneo ya kuoshea magari na maeneo ya huduma mbalimbali za kijamii.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari, Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Shinyanga, Angelina Magazi amesema mradi huo unajengwa ili kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara wilayani humo.
Amesema kuwa mradi huo utakapokamilika utagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja za Kitanzania.
Naye Mshauri wa Mradi huo, Godfrey Mkumbo amesema ujenzi wa majengo hayo ya kisasa utakamilika ndani ya miezi sita ukiwa umezingatia viwango vya kisasa.
Amesema mradi huo utakuwa na jumla ya maduka 54 yakiwa na huduma zote muhimu za supermarkets, migahawa na maeneo ya kuoshea magari.
Mradi huo unajengwa kwenye eneo la Bukondamoyo mjini Kahama, Shinyanga ilipo stendi mpya ya mabasi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...