Katika jitihada za
kuhakikisha jamii za Watanzania zinaendelea kunufaika na huduma bora za
teknolojia na mawasiliano nchini kote, Vodacom Tanzania PLC imezindua
kampeni mpya ijulikanayo kama ‘Zaidi ya Mtandao’ na kuwajulisha wateja
wake wapya kuwa sasa wanaweza kutuma na kutoa pesa bila ya tozo kwa
miamala chini ya shilingi 50,000.
Akizungumza kwa niaba ya
Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa Vodacom Tanzania Plc, wakati wa
uzinduzi uliofanyika katika soko la Mabibo jijini Dar es Salaam, Bi.
Brigita Shirima ameelezea kuwa kampeni hii mpya ni muendelezo wa namna
ambavyo kampuni hiyo yenye Mtandao Supa nchini inagusa maisha ya kila
siku ya Watanzania kwenye sekta tofauti za kijamii na kiuchumi kupitia
huduma na bidhaa bunifu za kidigitali.
Kampeni ya Zaidi ya
Mtandao inahamasisha Watanzania kujiunga na mtandao supa ulioenea nchi
nzima na wenye kasi ya 5G. Wateja pia watafurahia vifurushi vya bei
nafuu na huduma kemkem za M-Pesa.
“Ni furaha kubwa kuwajulisha
Watanzania na haswa wateja wapya kuwa sasa hakutokuwa na makato ya tozo
pindi watakapotuma na kupokea pesa chini ya shilingi 50,000. Wateja wetu
wapya wataanza kunufaika na huduma hii kuanzia leo ambapo tumezindua
kampeni yetu mpya inayojulikana kama ‘Zaidi ya Mtandao’ ambayo imekuja
na maboresho ya huduma na bidhaa zetu pamoja na ofa mbalimbali. Miongoni
mwa faida kwa mteja mpya wa Mtandao Supa wa Vodacom ni kurudishiwa
asilimia 15 ya gharama za bando pindi akinunua vifurushi kupitia
M-Pesa,” alisema Bi. Shirima.
Aidha, akifafanua zaidi kwanini ni
muhimu kwa wateja wa Vodacom kutumia M-Pesa kununua vifurushi,
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa hii ni katika harakati za kampuni hiyo
kuchangia utunzaji wa mazingira ikiwa ni dhumuni walilojiwekea sambamba
na lengo namba 13 la maendeleo endelevu (SDGs).
Mkurugenzi huyo
wa Biashara na Masoko alifafanua kuwa Vodacom Tanzania inajivunia
kuendelea kuboresha mtandao wake ambapo mwezi Septemba mwaka jana
walizindua huduma ya 5G yenye ubora, ufanisi, na iliyoenea nchi nzima
kwa shughuli binafsi na za kibiashara.
Akielezea
sababu moja wapo inayoifanya Vodacom kuwa ‘Zaidi ya Mtandao’ ni kwamba
mpaka sasa ina mawakala wa mauzo takribani 29,000 walioenea nchini kote
kuwahudumia Watanzania huku wateja wake wakinufaika na faida lukuki za
M-Pesa ikiwemo huduma za mikopo nafuu na upatikanaji rahisi wa ‘floti’
kuendeshea biashara zao.
Kwa upande wake Mkuu wa Kanda ya
Kaskazini wa kampuni hiyo, Bw. George Venanty, ameongezea kuwa uzinduzi
wa kampeni mpya ya ‘Zaidi ya Mtandao’ umefanyika kwa pamoja katika kanda
nyingine nne tofauti ambazo ni kanda ya ziwa, kanda ya Dar es Salaam,
kanda ya kati na nyanda za juu kusini, ambapo shughuli mbalimbali
zitaendelea na kuenea kwingineko kwa lengo la kuwafikia Watanzania wote
nchini.
“Vodacom inajivunia kuendelea kutoa huduma za teknolojia
na mawasiliano zinazokidhi mahitaji ya Watanzania wote nchini. Mimi na
timu yangu ya mawakala wa usajili tupo tayari kuipeleka habari hii nzuri
kwa wateja kwenye mitaa tofauti ya jiji la Arusha na viunga vyake
pamoja na mikoa ya jirani,” alisema Bw. Venanty.
Kampuni hiyo
inaamini kwamba washirika na wadau wake waliotapakaa nchini kote
wataendelea kuwaunga mkono kupitia ushirikiano walionao kwa miaka mingi
katika kuhakikisha Watanzania wote wanafikiwa na huduma bora na nafuu za
mawasiliano.
Vodacom imeendelea kuboresha huduma na bidhaa zake
kupitia ubunifu wa kidigitali kama vile kupata mikopo ya wateja binafsi
kupitia Songesha na M-Pawa, pamoja na VodaBima inayowawezesha kupata
bima kwa kuweka pesa kidogo kidogo kupitia M-Pesa kwenye simu zao za
mkononi.
Vile vile, kwa upande wa huduma kwa wateja, hizi
zimeboreshwa zaidi ili kumuwezesha mteja kujihudumia mwenyewe kupitia My
Vodacom App, kupiga simu, jumbe fupi, WhatsApp pamoja na kurasa rasmi
za mitandao ya kijamii ya kampuni hiyo.
Hii yote ni katika
kuonyesha jinsi ambavyo Vodacom inamthamini mteja wake na hivyo mbali na
huduma za mawasiliano, imejikita katika kubadilisha maisha yake kuptia
teknolojia na ndio maana tunasema Vodacom ni Zaidi ya Mtandao.Mkurugenzi
wa Biashara na Masoko wa Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa akifurahia
kwa pamoja na mawakala wa mauzo baada ya kuzindua programu maalum ya
tuzo kwa mawakala hao ikiwemo kujishindia safari ya kwenda Afrika ya
Kusini. Uzinduzi huo ni sehemu ya kampeni mpya inayojulikana kama ‘Zaidi
ya Mtandao’ uliofanyika jijini Dar es Salaam na mikoa mingine nchini
kote jana.
Mkuu
wa Kanda ya Mauzo ya Dar es Salaam wa Vodacom Tanzania, Bi. Brigita
Shirima akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya
‘Zaidi ya Mtandao’ kwa wateja waliojitokeza katika soko la Mabibo jijini
Dar es Salaam jana. Katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es
Salaam na mikoa mingine nchini kote jana, Vodacom iliwajulisha wateja
wake wapya kuwa sasa wanaweza kutuma na kutoa pesa bila ya tozo kwa
miamala chini ya shilingi 50,000.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...