Na Mwandishi Wetu


JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga limesema mtu mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 hadi 40 ameua baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira baada ya kutuhumiwa kuiba mahindi mabichi katika Shamba lililopo Kijiji cha Mwamalili MANISPAA ya Shinyanga.

Akizungunzia tukio hilo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Leonard Nyandahu amesema mtu huyo ameuliwa usiku wa kuamkia Aprili 4 mwaka huu baada ya kushambuliwa na wananchi wakimtuhumu kuiba mahindi mabichi shambani.

Amefafanua mtu huyo ambaye ameuawa hajafahamika jina lake wala Makazi yake lakini anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 hadi 40.

Katika tukio la pili , Kaimu Kamanda Nyandahu amesema linahusisha ugomvi kati ya Tumaini Malima mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa mtaa wa Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga wakigombana Yohana Daniel wakiwa wanakunywa pombe kwenye Bar Heinken iliyopo kambarage mjini Shinyanga.

Watu hao wote wawili walifika kituo cha polisi na kupatiwa hati ya matibabu (PF3) kwa ajili ya matibabu huku akieleza kwamba Tumaini Malima amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga .

Amesema Yohana Daniel yeye amekimbia na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga wanaendelea na jitihada za kumtafuta zinaendelea na mara baada ya kumkamata atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayo mkabri.

Aidha Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Leonard Nyandahu ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi matukio ya uhalifu yanapotokea.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...