Na Mdau wa Maendeleo ya Viwanda nchini.
Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia kampuni inayodaiwa kujiita Chalinze Cement na nilichokiona kinachekesha. Je, unajua kwamba kampuni hii haimiliki ardhi yoyote ambayo inaweza kuchimba mawe ya chokaa kwaajili ya uzalishaji wa simenti? Pia haina hata chapa wanayodai kuwa nayo. Hawaingizi hata sementi nchini kupitia bandari zetu zozote za Tanzania.
Kitu pekee nilichoweza kupata kwa wanachi na watumiaji wa bidhaa ya saruji kuhusiana na kampuni hii ni duka la ujenzi na rangi liliopo Kisutu mkoani Dar es Salaam.
Hakuna kingine! Ndivyo ilivyotokea kama nilipouliza kuhusu kikundi hiki cha kutetea walaji nchini sikupata ukweli wala kitu chochote kuhusu wao.
Hakina wanachama, hakina ofisi, na hata hakina usajilih ivi najiuliza wanapataje haki ya kuwakwamisha watanzania wenzao kwenye uwekezaji huu mkubwa wa dola za kimarekani milioni 500?
Niwaombe kitu waandishi wezangu nawapa changamoto ya mmoja wenu kuchapisha picha za wafanyakazi wa Chalinze Cement au picha ya mfuko wao wakuhifadhia simenti, hata picha ya leseni yao ya uchimbaji madini ya chokaa.
Hata kama hawajaanza uchimbaji Chapisheni hayo ili wananchi waelewe kuwa wao ni wawekezaji nchini.
Hivyo hivyo kwa Chama cha kuwatetea walaji nchini (TCAS). Elezeni idadi ya wanachama wanu Je ni kesi gani wamewahi kushinda huku wakiwatetea walaji nchini?
Kwa hivyo nashangaa… Inakuwaje wapate nafasi ya kuchelewesha uwekezaji wa dola milioni 500 kati ya kampuni ya Twiga na Tanga Cement.
Ucheleweshaji uliochukua zaidi ya mwaka na nusu Je? sisi Watanzania, tungeweza kuokoa kiasi gani cha fedha kwa kuwa na fedha hizo nchini kwetu?
Nimesikia tetesi kwamba wanajaribu kuweka ugumu kwenye uuzwaji huu kwa kusababisha ucheleweshaji zaidi. Lakini ni wazi kwamba kampuni ya Twiga na Tanga Cement hazitasimama kwenye hilo.
Home
HABARI
AONAVYO MDAU WA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI JINSI MAKAMPUNI FEKI YANAVYOHUJUMU UCHUMI WA TANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...