Kampuni ya usafiri kwa njia ya Taxi-mtandao Bolt inafanya kazi kwa ukaribu na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) katika juhudi zetu za kuboresha usalama na viwango katika soko la taxi-mtandao. Tunashukuru kwa hizi hatua kwani zitaboresha usafiri wa taxi-mtandao kote nchini, na pia kutatua masuala yanayoathiri madereva na jumuiya ya abiria.

Akizungumza kwenye taarifa hiyo Meneja Mkazi wa Bolt, Charles Matondane alisema, Bolt ingependa kusisitiza kwamba ina ofisi moja tu iliyosajiliwa Dar es Salaam. Bolt ingependa kusisitiza kwamba haina ofisi nyingine nchini Tanzania na ingependa kushauri umma kutofanya shughuli yoyote rasmi na watu wasioidhinishwa.

Tunawatahadharisha madereva wasifanye shughuli au kujihusisha na mawakala wowote ambao hawajaidhinishwa au watu wanaodai kuwakilisha Bolt. Kwa hali yoyote, tunawahimiza madereva kuwasiliana nasi mara moja ili tuweze kusaidia kwa hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya watu hawa kwa polisi wa eneo hilo. 

Pia tumeripoti maeneo mawili katika vituo vya Polisi vya Kati jijini Dar es Salaam ili kuwachukulia hatua watu hao wasio halali. Bolt pia inafanya kazi na mamlaka husika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaodai kuwa mawakala walioidhinishwa kuwasaidia usajili madereva kwenye Tovuti/Programu ya kampuni.

Tungependa pia kusisitiza kwamba Bolt haiwatozi kiasi chochote madereva kufanya usajili kwenye Tovuti/ Programu ya kampuni, kwa hivyo, madereva hawapaswi kumlipa mtu yeyote ili kupata huduma ya usajili katika Tovuti/Programu ya kampuni kwani Bolt haitawajibishwa kwa miamala yoyote kama hiyo.

Bolt pia inafahamu baadhi ya madereva ambao kwa ulaghai wamekuwa wakitumia programu haramu inayoitwa “Zuzu”, ambayo inawalaghai baadhi ya wateja wetu kwa kuwatoza nauli zaidi ya safari. Tungependa kusema kwamba utumiaji wa programu mbadala au viraka kwa madereva kwenye soko ni kinyume cha sheria na Bolt haikubaliani na tabia kama hiyo.

Bolt imetoa taarifa za madereva hao waliofanya makosa hayo LATRA na Kituo cha kati cha polisi kwa hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya madereva hao. Tumekuwa tukifanya kazi na kampuni za mifumo ili kuhakikisha programu hizi haramu na udukuzi wa simu janja unapunguzwa ili kuhakikisha takwimu na taarifa zao za GPS hazitarekebishwa ili kupandisha bei ya safari. 

Kwa sasa Bolt itafungia dereva yeyote mwenye viashiria au anayetumia programu hizi haramu na ingependa kuwashauri madereva wote kuhakikisha kuwa wanatumia matoleo mapya ya programu ya Bolt.

Bolt bado inania ya kuimarisha uhusiano wa madereva wake katika soko la Tanzania na ili kusimamia matarajio ya madereva, mipango inaendelea ya kufungua Kituo cha Uhusiano na Madereva jijini Dar es Salaam Mei mwaka huu ili kuwasaidia madereva wenye matatizo yoyote. Tunashahuku na Kituo chetu kipya cha Uhusiano wa Madereva kilichopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam, na tutawakaribisha LATRA na jumuiya yetu ya madereva kwenye kituo chetu baadaye mwezi huu.

Hatimaye, Bolt imejitolea kuendelea kutoa huduma za Taxi-Mtandao nchini Tanzania na kutengeneza fursa za ujasiriamali zinazowezesha watu wengi zaidi kujikimu kimaisha.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...