Na Dotto Mwaibale, Singida
JESHI la Polisi mkoani Singida linamshikilia John
Musoma (30) Mkazi wa Kijiji Cha Nkonko wilayani Manyoni kwa tuhuma za kumua
mtoto wake na kumjeruhi mwingine kwa kumpiga fimbo kichwani.
Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Stella
Mutabihirwa, katika taarifa yake jana kwa vyombo vya habari, alisema mtuhumiwa
huyo alikamatwa Mei 4, 2023 kwa kumuua mtoto wake aitwaye James Musoma (6) na
kumjeruhi mwingine Joseph Musoma (8).
Kamanda Mutabihirwa alisema sababu za mtuhumiwa
huyo kuwapiga watoto wake hao ni baada ya kuchelewa kufika shambani kufukuza
ndege wanaoshambulia zao la iweke.
Alisema kutokana na tukio hilo mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika.
Kamanda Mutabihirwa ametoa wito kwa wazazi na
walezi kuacha vitendo vya ukatili vinavyoambatana na vipigo kwa watoto wao
kwani vinaweza kugharimu maisha ya watoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...