Nahodha wetu amejitolea kwa dhati kuwatumikia Wazanzibari na kuinua hali ya Zanzibar bila kujali dini, kabila na chama. 

Katika kuleta mageuzi hayo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameanza kuibadilisha Zanzibar katika nyanja mbalimbali ili kuinua maisha ya wazanzibari

1. Michezo: amelenga kuimarisha sekta ya michezo kwa kuwekeza katika ujenzi wa viwanja vipya na kuboresha vya zamani, kuendeleza talanta za vijana na kuboresha mazingira ya michezo.

2. Elimu: Amejenga Skuli za Msingi na Sekondari pamoja na Vituo vya elimu jumuishi (kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum) pamoja na kuongeza mishahara ya Waalimu.

3. Afya: Ameboresha huduma za afya kwa kujenga vituo vya afya na hospitali kwa ngazi zote ikiwemo kuimarisha miundombinu ya hospitali, kutoa mafunzo ya kina kwa wafanyakazi wa afya, na kuongeza upatikanaji wa huduma za matibabu.
 

4. Miundombinu: kuboresha miundombinu ya barabara kuanzia barabara za ndani, Flyover, ujenzi wa Airport mpya pemba na unguja.
 

5. Uwekezaji: Ameongeza fursa za uwekezaji na kukuza uchumi wa Zanzibar kwa kuvutia wawekezaji wa ndani na nje na kuboresha mazingira ya biashara.

6. Uvuvi: Amewawezesha wavuvi kwa kuwapa maboti yenye uwezo wa kwenda bahari kuu ambayo yana vifaa vya Gps na Fish finder vifaa ambavyo vina uwezo wa kutafuta samaki pamoja na kuwajengea diko la samaki

7. Vituo vya wajasiriamali: amejenga vituo vya wajasiriamali kwa lengo la kuwaondoa wachuuzi kutoka mfumo genge na kuwaingiza katika mfumo soko.

8. Uwezeshaji: Ametoa mikopo isiyo na riba kwa wajasiriamali wadogo wadogo na makundi mbalimbali pamoja na fursa za mafunzo ili kujiajiri na kujikimu kimaisha.

9. Maji safi na Salama: Anapigania kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa kila mwananchi kwa kujenga matangi na kuboresha miundombinu ya maji vijijini na mijini.

10. Mishahara kwa wafanyakazi: amechukua hatua muhimu za kuimarisha hali za maisha ya wafanyakazi wa Serikali na wastaafu.

Ni wazi kuwa Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi ameonyesha azma thabiti ya kuhakikisha maendeleo yanayomgusa kila mmoja katika jamii ya wazanzibari kupitia sera zake na mipango ya maendeleo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...