Na Jane Edward, Arusha

BAADHI ya wawakilishi kutoka Mtandao wa Wakulima Wadogo wa Mashariki na Kusini mwa Afrika(ESAFF),wamesema kwa mujibu wa utafiti uliofanyika umebaini kwamba ni asilimia 30 tu ya ardhi inayotumika katika shughuli za kilimo kwa nchi za ukanda wa Juimuiya ya Afrika mashariki(EAC).

Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Kundi kutoka Shirika la Association of Women in Agriculture in Kenya(AWAK), Julius Mundia,wakati wa kongamano la kwanza la Jumuiya ya Asasi za Kiraia za Afrika Mashariki,lililofanyika kwa siku tatu jijini Arusha.

Mundia,anasema ufatifi huo,umebaini kwamba asilimi 70 ya ardhi katika nchi hizo,haitumiki na zimekaa bure huku asilimia 30 ndizo zikitumiwa na wakulima kwa ajilii ya shughuli ya uzalishaji wa chakula.

Ameongeza kuwa kutokana na kiwango kikubwa cha ardhi kutokutumika kwa shughuli za kilimo nchi hizo,zinakabiliwa na uhaba wa upatikanaji wa chakula na chakula kinachopatikana hakitoshelezi mahitaji ya wananchi wake.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Kilimo na Usalama wa Chakula kutoka EAC,Fahari Marwa,alisema jumuiya hiyo inasaidia nchi wanachama katika mambo mbalimbali ikiwamo kuweka miongozo ya pamoja,sera na sheria ambazo zitasaidia kukuza sekta ya kilimo.

Alisema suala la bajeti kuwa ndogo katika sekta ya kilimo limekuwa likizungumzwa lakini jumuiya hiyo imekuwa ikiwasisitiza nchi wanachama asilimia 10 za bajeti yao kubwa kupeleka kwenye kilimo,”alisema.

“Takwimu zinaonyesha nchi nyingi hazitengi kiasi hicho cha asilimi 10 lakini EAC tumekuwa tukihimiza zifanye hivyo kwa ajili ya kuinua kilimo kwa kuwa ndio uti wa mgongo na tunaamini zitaendelea kutekeleza wajibu huo.

Naye Mwenyekiti wa ESAFF,Baliraine Hakim,alisema mkutano huo umewakutanisha wakulima wadogo kutoka mashariki na kusini mwa Afrika kujadiliana na kuangalia namna nchi hizo zitaweza kuweka mipango ya kuongeza fedha kwenye kilimo na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania,Apolo Chamwela(MVIWATA),alipingana na utafiti huo,akidai kuwa ardhi kubwa inatumiwa na wakulima wakubwa badala ya wadogo.

Aidha alisema utafiti huo,umelenga kuaminisha watu kuwa ardhi haitumiki ili wahusika wapate nafasi ya kuwaleta wawekezaji kwenda kutumia maeneo makubwa na wanachi kukosa sehemu za kufanya shughuli za kilimo

Mkurugenzi Mtendaji ESAFF Joe Mzinga akizungumza na washiriki wa Mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...