Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Camillus M.Wambura IGP akiwa na ujumbe wa Maofisa watano kutoka Jeshi la Polisi Tanzania leo Mei 15,2023 wameanza rasmi ziara ya kikazi Nchini Ireland ambapo ametembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Ireland "An Garda Síochána" na kukutana na Deputy  Commissioner Anne Marie McMahon.Wameweza kubadilishana uzoefu wa namna ya kubaini,kuzuia na kutanzua  makosa ya jinai hususani Ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji dhidi ya watoto.

Pia walipata fursa ya kujadili namna ya kushirikiana kwenye eneo la mafunzo kwa maafisa na askari kati ya Jeshi la Polisi Ireland na Jeshi la Polisi Tanzania. Picha na Demetrius Njimbwi wa Jeshi la Polisi Tanzania.


 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...