Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi-Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Nchini Tanzania limesema kuwa limeona mjadala katika mitandao ya kijamii ikuhusiana na kifo cha Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma Bi. Nusura Hassan Abdallah kilichotokea huko Mkoani Kilimanjaro.

Akitoa taarifa hiyo leo mei 06,20223 msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi David Misime amesema kuwa taarifa hizo zimekuwa zikihusisha kifo hicho na ajali iliyotokea Jijini Dodoma aprili 26,2023 ikimhusisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi (Afya) Mhe.Dkt. Festo Dugange ambapo zinadaiwa zimetokana na kipigo kutoka kwa mpenzi wake.

Msemaji wa Jeshi hilo amebainisha kuwa Jeshi la Polisi Tanzania lingependa kutoa ufafanuzi kuwa, Polisi Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kuona taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na sababu zinazotolewa,wameshaanza uchunguzi kwa watu mbalimbali,hospitalini alikotibiwa binti huyo ambapo amesema wanashirikisha Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali,Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na wadau wengine wa haki jinai.

Aidha Jeshi hilo limetoa wito kwa mtu yeyote mwenye taarifa zilizosahihi na zenye ukweli asisite kutoa taarifa hizo ili kuharakisha uchunguzi wa tukio hilo.

Pia SACP Misime amesema kuwa Jeshi la Polisi Nchini linasisitiza kuwa Uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika taarifa kamili ya kilichobainika kitatolewa kwa umma na kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu za Nchi.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...