Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Mei 6, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, amepokea taarifa ya Kamati aliyoiunda kuchunguza tukio la kukatika umeme katika uwanja huo wakati wa mechi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Dar es Salaam Young Africa ( Yanga) dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Baada ya kupokea taarifa hiyo, Waziri Dkt. Chana amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara Ndg. Saidi Yakubu kufanyia kazi taarifa hiyo ikiwemo kuchukua hatua zinazostahili kulingana na taarifa hiyo.Tukio hilo la kupokea taarifa lilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu,Bw Nicholas Mkapa.

Kamati hiyo imeongozwa na  Mwenyekiti  Mhandisi Keneth Boymanda kutoka Shirika la Umeme Tanzania  (TANESCO), ikiwa na Wajumbe kutoka  Wakala wa Majengo nchini TBA,  na baadhi ya watumishi wa wizara.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...