Na Mwandishi Wetu, DODOMA

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi amesema serikali inazingatia watanzania wote wanaojenga nchi yao na imeweka utaratibu wa kupata pensheni kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa waajiriwa na waliopo kwenye sekta isiyo rasmi.

Mhe.Katambi ameyasema hayo Mei 2, 2023 bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Magu (CCM),l Mhe.Boniventura Kiswaga ambaye amehoji lini serikali italipa kiinua mgongo kwa wazee ambao hawajawahi kuajiriwa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Katambi amesema kiinua mgongo ni malipo ambayo hulipwa na mwajiri pindi mfanyakazi wake anapostaafu kufanya kazi.

Mhe.Katambi amefafanua kuwa, kutokana na kuwepo kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii mwajiriwa na mwajiri huchangia, mfanyakazi hulipwa pensheni badala ya kiinua mgongo na hupokea mafao ya mkupuo mara anapostaafu na baadae kuendelea kulipwa pensheni ya kila mwezi kwa maisha yake yote na kwasasa hakuna mfumo wa kulipa kiinua mgongo kwa wazee ambao hajawahi kuajiriwa.

Hata hivyo, amesema kwa watu waliopo kwenye sekta isiyo rasmi ikiwamo wajasiriamali, wakulima na wafugaji, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) ndio wenye jukumu la kushughulikia sekta hiyo na umeanza kukusanya michango kwa kuwatambua waliyo kwenye makundi hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...