Mabondia Yusuf Changalawe (Captain) na Alex Isendi (kulia) kuanza katika mzunguko wa 64 kuipeperusha bendera ya Tanzania kesho Jumanne katika mashindano ya ngumi ya IBA UBINGWA WA DUNIA TASHKENT 2023 katika uwanja wa Humo Arena, mini Tashkent, Uzbekistan
Mabondia hao watazipiga katika uzito wa Light welterweight 63.5kg bout no. 77 Alex Isendi (Blue) vs Usmonov Bakhodur kutoka Tajikistan, na Light heavyweight 80kg bout ]no.85 Yusuf Changalawe (Blue) vs Naveriani Otar kutoka Georgia.
Kwa mujibu wa Ofisi ya rais wa BFT, mapambano yao yatafanyika session ya 3A jioni majira ya saa 12 jioni muda wa Tashkent (Tanzania saa 10 jioni)
\Taarifa ya awali ya BFT inaeleza kwamba ratiba ya mashindano ya ngumi ya IBA UBINGWA WA DUNIA - TASHKENT 2023 kwa wanaume imetoka baada ya kikao cha upangaji wa ratiba katika hoteli ya Hilton, Tashkent, Uzbekistan, na kwamba jumla ya mabondia 539 (Idadi ya kihistoria) kutoka mataifa 107 wameandikishwa kushiriki katika uzani 13.
Tanzania inawakilishwa na Mwalimu Mkuu Samwel Kapungu "Batman", Yusuf Changalawe, Raisi BFT Lukelo Willilo, na mabondia Kassim Mbundwike, Alex Sita na Alex Isendi.
Ratiba kamili kwa Tanzania ni kama ifuatavyo;
Jumanne 2-05-2023
1. Light welterweight 63.5 Alex Isendi (Blue) vs Usmonov B kutoka Tajikistan.
2. Light heavyweight 80kg Yusuf Changalawe (Blue) vs Naveriani O kutoka Georgia.
Jumatano 03-05-2023
3. Light middleweight 80kg Kassim Mbundwike (Blue) vs Yeasungneon P kutoka Thailand.
Alhamis 4-05-2023
4. Super heavyweight 92+
*Alex Sita Sulwa* (Red) vs Bondia kutoka Algeria.
Mashindano yameanza rasmi leo Jumatatu tarehe 1-05-2023 huku Tanzania ikishiriki kwa mara ya 4.
Pia kutakuwa na zawadi za pesa kwa washindi katika kila uzani 13 kama ifuatavyo.
1. Dhahabu na $200,000 (Tzs 470,000,000)
2. Fedha na $100,000 (Tzs 234,000,000)
3&4. Shaba na $50,000 (Tzs 116,000,000)
Mungu ibariki Ngorongoro Black Rhinos (Faru weusi wa Ngorongoro) Mungu ibariki Tanzania 🇹🇿 🥊
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...