Na Victor Masangu,Kibaha
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha Selina Koka katika kuunga juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kuboresha sekta ya michezo anatarajia kuanzisha mashindano ya mchezo wa netiboli katika kata zote 14.
Selina ameyasema hayo wakati wa ziara ya kikazi ya Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini katika kata za Pangani na Tangini ambayo imehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama kutoka ngazi mbali mbali.
Aliongeza kuwa anatambua umuhimu wa sekta ya michezo na ndio maana ameamua kuanzisha mashindano hayo katika kila kata ambayo yataweza kuibua na kukuza vipaji kwa wanawake katika kila kata na baada kuweza kupata timu ya jimbo.
Selina alisema katika kufanikisha shindano hilo ametoa vifaa mbali mbali vya mchezo wa netiboli ikiwemo jezi pamoja na mipira ili kuweza kuunda timu hizo za kata.
"Lengo langu kubwa ni kukuza na kuinua mchezo wa netiboli na kwamba nimetoa jezi na mipira katika kata mbali mbali na nia yangu zaidi ni kuanzisha mashindano ambayo yatakwenda kwa jina la Selina Koka Cup na maandalizi tayari yameshaanza,"alisema Selina.
Kwa Upande wake Diwani wa kata ya Pangani Mfaume Kalanguti amemshukuru Mbunge Koka kwa kuweza kuleta chachu ya maendeleo katika nyanja mbali mbali hususan sekta ya michezo.
Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mji Elina Mgonja alibainisha kuwa kuanzishwa kwa mashindano hayo kutaweza kusaidia kuibua vipaji mbali mbali vya wanawake ambao wanatoka katika kila kata.
Aidha alisema wanawake katika kata za Pangani na Tangini wanapaswa kuanzisha timu za michezo ambayo itaweza kuwapa fursa zaidi ya kukiimarisha chama na kumpongeza Selina Koka kwa juhudi zake za kuwasaidia wanawake kiuchumi.
Ziara ya Mwenyekiti wa UWT ambayo imefanyika katika kata mbili za Tangini pamoja Pangani imelenga zaidi katika kuangalia uhai wa chama pamoja na kuimarisha Jumuiya kuanzia ngazi za matawi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...