Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAMIA ya waombolezaji jijini Dar es Salaam pamoja na mikoa jirani wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan wametoa salamu za mwisho kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe aliyefariki dunia Mei 12 mwaka huu katika Hospitali ya Kairuki.

Rais Samia ameongoza waombolezaji katika kutoa salamu za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Membe katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo Mei 14 mwaka huu 2023.Mbali ya Rais Samia viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na viongozi wengine waliokuwepo kwenye kuaga mwili wa marehemu Membe.

Pia walikwepo viongozi wa vyama vya siasa mbalimbali, viongozi wastaafu , wakuu wa idara na taasisi pamoja na wananchi na wakati wote katika viwanja hivyo majonzi na simanzi vilikuwa vimetawala muda wote.Ukweli kifo cha Membe kimesikitisha wengi.

Akizungumza mbele ya waombolezaji wakati akitoa salamu za pole na rambirambi kwa familia ya Membe, ndugu , jamaa na marafiki,Rais Dk.Samia amesema katika mambo ambayo mwanadamu hawezi kujipangia ni siku ya kuzaliwa au kuja kwake duniani.

“Hata kama utakuja kwa njia yoyote ile ya upasuaji na daktari akapanga siku au mama atapanga tarehe ya kufanyiwa upasuaji kama Mungu hakutaka tarehe ile itatokea jambo utakuja kwa tarehe nyingine…

“Lakini siku ya kurudi kwa Mungu siku ya kufa binadamu hatuwezi kujipangia, leo tumekutana hapa kumuaga mpendwa wetu Bernard Kamiulis Membe ambaye ameitika amri ya kurudi kwa Mola wake bila shaka wote tuna huzuni na mshituko wa taarifa za kifo chake kilichotokea Mei 12 mwaka huu hapa Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi,”amesema Rais Samia.

Ameongeza yeye mwenyewe , familia yake, Serikali na Watanzania wote wanaungana na wengine kutoa salamu za pole na rambirambi kwa mjane wa marehemu , watoto wa marehemu Cecilia, Richard na Denis, ndugu,jamaa,marafiki , Wana lindi na wote walioguswa na msiba huu mzito

“Kifo cha ndugu Membe kimesikitisha wengi ndani na nje ya nchi ya mikapa yetu kwani alikuwa mashuhuri na mwanadiplomasia mahiri.Naelewa machungu ya wanafamilia kutokana na msiba huu mkubwa lakini familia huu si msiba wenu peke yenu ni msiba wetu sote …

“Ingawa athari na machungu ya msiba huu kwa kiasi kikubwa kitakuwa upande wenu kwa kuwa mmeondokewa na mtoto kwa wazazi wake, au ndugu kwa wazazi wake na mume wa mjanae na baba wa Cecilia, Richard na Denis, kwa babu, hakika nguzo kuu imedondoka , Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu, awape subira katika kipindi hiki kigumu mnachopitia.”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernard Kamilius Membe katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa pole kwa Familia ya aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernard Kamilius Membe mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernard Kamilius Membe mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na waombolezaji kabla ya kuwaongoza kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernard Kamilius Membe katika viwanja vya Karimjee tarehe 14 Mei, 2023.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...