Kaimu Mkuugenzi mkuu wa (TPHPA) Profesa Joseph Nduguru akizungumza na waandishi wa habari akiongea na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya siku ya afya ya mimea duniani inayoadhimishwa mei 12 kila mwakaDkt.Benignus Ngowi Afisa ukaguzi na Afya ya Mimea,afya utafiti mwandamii ,akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimishi ua siku ya Afya ya mimea.
Wakwanza kushoto ni Profesa Eliningaya Kweka akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimishi ya siku ya Afya ya mimea inayoadhimishwa kila mwaka mei12
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika ukumbi wa Mamlaka ya Afya mimea na Viuatilifu Mkoa wa Arusha
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika ukumbi wa Mamlaka ya Afya mimea na Viuatilifu Mkoa wa Arusha
NA.VERO IGNATUS,ARUSHA
80% ya chakula cha binadamu kinatoka kwenye mimea ,98% ya Oksgen tunayotumia inatoka kwenye mimea lakini mimea hiyo hiyo inakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kuwepo na visumbufu kama wadudu wahaibifu ,magonjwa pamoja mabadiliko ya tabia nchi kama vile ukame pamoja na uhaibifu wa mazingia hali inayosababisha kuwa na upungufu wa chakula pamoja na kuharibika kwa mazingira.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuugenzi mkuu wa Mamlaka ya Afya ya mimea na viuatilifu Mkoani Arusha (TPHPA) Profesa Joseph Ndunguru ,wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya siku ya afya ya mimea duniani inayofanyika kila mwaka mei 12,ambapo alibainisha Kwa nchi ya Tanzania afya ya mimea ni muhimu sana kwasababu tukiwa na udhibiti wa visupufu mahiri,tutaweza kuongeza tija,ajira na pia kupunguza umasikini na kukuza uchumi wa nchi kwani malighafi ya vviwanda yataongezeka kwasababu 60%ya malighaafi yanayoingia kwenye viwanda yanatokana na sekta ya kilimo
Prof.Ndunguru alisema kuwa kuwepo kwa wadudu wahaibifu magonjwa na mabadiliko ya tabianchi kama vile ukame uchomaji misitu,vinasababisha kupungua kwa chakula hivyo upo umuhimu wa kutunza afya ya mimea ili kufikia malengo.
Aliongeza kuwa Katika kuadhimisha siku hii Mamlaka ya Afya Viuatilifu (TPPA) nchini imesema kuwa mwaka 2022-2023 kuimarisha afya za mimea jumla ya shehena za vipando 189 zilikaguliwa na zilionekana zimekidhi viwango vya matakwa ya afya ya mimeana hivyo kuruhusu biashaa kufanyika sambamba nachunguzi za sampuli 103 za mahabara na vitalu nyumba na zilikidhi viwango,pamoja na kupokea jumla ya maombi 762 ya vibali vya kuingiza vipando nchini ambapo vibali 756 kwa maana ya 99.2% vilitolewa.
‘’Pia tuliweza kutoa mafunzo kwa 3100 na maafisa ugani 900katika udhibiti wa mdudu kanitangaze,lakini pia katika kudhibiti viwavijeshi mamlaka ilitoa jumla ya lita za viwatilifu 81563 na kusambazwa katika halmashauri 57 za mikoa ya lindi pwani Morogoro geita manyara kilimanjaro,lita 561 za aina mbili nza viwatilifu pia zilisamazwa katika halmashauri ya wilaya ya kilosa,jumla ya wakulima 2987 na maafisa ugani 16 katika halmashauri ya kilombeo walipatamafunzo namna ya kudhibiti visumbufu vya mimea,huku ukaguzi wa mazao tani mil 5,343,380 za mazao na nafaka za mizizi mbalimbali mipakani,bandarini na viwanja vya ndege ,jjumla vya vyeti 29,033 na usafi wa mimea vilitolewa na kuruhusu biashara ya mazao kufanyika’’
Mamlaka iliweza kufanikiwa kudhibiti milipuko ya panya katika kukoa eneo hekari 122190,ili kudhibiti inzi wa matunda jumla ya lita vya viwatilifu 585 na kusambazwa katika wilaya ya mbalimbali ikiwemo muheza,pia tulidhibiti makundi ya kwelea 2,027,000 na kufanikiwa kuokoa hekari1056 ambazo zingekuwa zimeheribiwa,pamoja na kudhibiti nzigena kuokoa jumla ya hekari 195,000,upatikanani wa viwatilifu bora jumla ya viwatilifu vipya jula ya 409 na kampuni 198 vilisajiliwa katika kipindi hicho ,vibali 10324ya kuingiza nchini shehena za viwatilifu vilitolewa.jumla ya vibali 802 vilitolewa kwa wafanyabishara wa viwatilifu.
“Kauli mbiu ya Siku ya afya duniani mwaka huu inasema afya ya mimea kwaajili ya kupunguza umaskini njaa,kulinda mazingiara , kukuza uchumi wanchi zetu ,sisi afya ya mimea tunaungana na wenzetu duniani kusheherekea siku hii lengo kubwa ni kuhabarisha umma juu ya kutunza afya ya mimea ili tuweze kuyafikia malengo”alisema pro.Ndungu
Kwa upaande wake Mkurugenzi wa afya ya mimea ambaye pia ni Afisa ukaguzi wa mimea na afya ya mimea Dkt.Benignus Ngowi alisema jukumu la taasisi yao ni kulinda taifa la Tanzania dhidi ya uingiaji wa visumbufu kutoka nje yan chi dhidi ya kusambaa kutoka eneo mmoja la nchi Kwenda eneo lingine la ndani ya nchi hadi nje yan chi na kwa muktadha huo huo Tanzania sio kisiwa jukumu lao lingine ni kuangalia bidhaa ambazo zinazalishwa na kuingizwa kutoka nje ya nchi na zinazokwenda nje hazina visumbufu kwa mimea ili kulinda masoko ya ndani yan chi pamoja na nje ya nchi
Alibainisha kuwa pia wanafanya kazi ya ukaguzi wa mazao ,mimea ,vipando vyote ambavyo kwa njia moja ama nyingine vinaingizwa Tanzania kwa madhumuni ya kibiashara ,kitafiti,msaada wa aina yeyote ile wanahakikisha havina visumbufu kwa maana havina wadudu waharibifu wa mazao yetu au vimelea vya magonjwa
Aliwasihi wananchi hususani wafanyabiashara na wakulima iwapo wakitaka kuingiza mazao wapiti katika taasisi yao kupata vibali ili kuepuka usumbufu na kusaidia kuepusha kuingiza vimelea au vidudu na visumbufu viatarishi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...