Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Manyara  watafanya upimaji na matibabu ya moyo kwa wananchi wa mkoa wa Manyara. Upimaji huo utaenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Shinikizo la Juu la Damu Duniani yatakayofanyika  tarehe 17/05/2023.

Upimaji huo utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia tarehe 15/05/2023  hadi tarehe 19/05/2023  saa mbili kamili asubuhi mpaka saa 10 kamili jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Manyara.

 

Kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na  kufuata mtindo bora wa maisha ambao utawasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

 

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapohapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi yetu.


Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayebainika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa namba 0768408984 Vailine Osward na 0714956529 Abubakar Mjaka.

 

“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...