NA FARIDA MANGUBE MOROGORO

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa amesema ni vyema wadau wa maendeleo kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita kulinda vyanzo vya maji kutokana na umuhimu wake katika uzalishaji wa umeme.

Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa Kwanza wa wabia wa maendeleo na nishati toka Nchi za sweden, Norway, Ufaransa, jumuiya ya Ulaya na benki ya dunia ulio fanyika Mjini Morogoro.

Amsema ni jambo la kupongeza pale wadau wanapotambua mchango WA Serikali na kuendelea kuunga mkono ili kumaliza kabisa changamoto ya nishati nchini kupitia wakala wa nishati vijijini (REA)

Nao wadau wa maendeleo akiwemo Stephene Mwakifimba Mratibu wa miradi ya nishati na mazingira, ubalozi wa Sweden amesema wana imani kubwa na serikali ya awamu ya sita hivyo kubainisha mipango yao ambayo wanaamini itazaa matunda kwa kushirikiaana na wakala wa nishati vijijini (REA)

Mkurugenzi Mkuu wakala wa nishati vijijini, REA Mhandisi Hassan Saidy amesema wao kama REA wamejipanga kuhakikisha wananchi waishio vijiji wanapata Huduma ya Nishati ya umeme itakayosaidia kuinua uchumi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.




 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...