NA FARIDA MANGUBE.
Zaidi
ya wakazi 6,900 wa kata ya Mbingu Halmashauri ya MLIMBA mkoani Morogoro
wanatarajiwa kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na
Salama utakapo kamilika mradi mkubwa wa Maji Mbingu ambao kwa awamu ya
Kwanza unagharimu Takribani shilingi Milioni 760.
Mradi huo
unaotekelezwa na Serikali chini ya Wakala wa Maji Safi na usafi wa
Mazingira vijijini (RUWASA) ni Kati ya Miradi sita iliyopitiwa na Mwenge
wa Uhuru mwaka 2023 kwenye halmashauri ya MLIMBA na kuwekewa jiwe la
msingi na kiongozi wa Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Abdalla
Shaib Kaim.
Akisoma Taarifa ya Mradi wa Maji Mbingu Kaim Meneja
RUWASA wilaya ya Kilombero Mhandisi Florence Mlelwa amesema mradi huo
umefikia asilimia 95 katika utekelezaji wake na utakapo kamilika
utamaliza kabisa shida ya maji katika eneo Hilo na kuwawezesha wakazi
wake kuendelea na shughuli za uzalishaji.
Akiwa katika Mradi wa
maji Mbingu kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdulla Shaib
Kaim amesema ameridhishwa na utekelezaji wa Mardi na matumizi ya fedha.
"Niwapongeza
Sana ndugu zangu RUWASA kwa kazi kubwa na zuri unayoifanya ya
kuhakikisha wananchi waishio vijiji wanapata maji Safi na salama.alisema
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Awali Mkuu wa Mkoa
wa Morogoro ,Fatma Mwassa amesema Bil. 12.1 zimetumika katika
kutekelezaji wa miradi 68 itakayotembelewa Mbio za Mwenge wa Uhuru
katika Halmashauri 9 za Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa Akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendegu, Halmashauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero Meneja wa RUWASA wilaya ya Kilombero Mhandisi Florence Mlelwa akisoma Taarifa ya Mradi wa Maji Mbingu mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdulla Shaib Kaim ( hayupo pichani)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...