-Kuelekea wiki ya Wafamasia Duniani.

Na. WAF - Dodoma

Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daudi Msasi amesema kuwa mwelekeo wa Wizara ya ni kuhakikisha huduma za afya zinazotolewa katika vituo vyote nchini hasa huduma za dawa zinaboreshwa ili wananchi wa hali zote wanufaike na huduma hizo.

Bw. Msasi amebainisha hayo leo Juni 10, 2023 alipotembelea katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General) katika Famasi ili kujionea hali ya upatikanaji wa dawa ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya wiki ya Famasi yenye kilele chake Juni 16 Jijini Dodoma, huku kauli mbiu ikiwa "Famasi ni nguzo ya mfumo wa huduma za afya ulio madhubuti, thabiti na bora".

"Mwelekeo wa Wizara ya Afya ni kuhakikisha kwamba tunaimarisha ubora wa huduma za afya kwa wananchi na ndio lengo kubwa." Amesema Bw. Daudi Msasi.

Amesema, upatikanaji wa dawa ni nguzo muhimu katika suala la ubora wa huduma, hivyo ameishukuru Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kutosha kwenye eneo la dawa, miundombinu, vifaa na vifaa katika vituo vyote nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora katika vituo vyote.

Aidha, Bw. Msasi amewashukuru Wafamasia wote nchini kwa kuendelea kujitoa katika kutimiza majukumu yao ikiwemo katika kusimamia upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma na eneo la elimu kwa wananchi ili kuongeza matumizi sahihi ya dawa na kuondoa changamoto ya usugu wa vimelea vya maginjwa dhidi ya dawa.

Nae, Kaimu Mkuu wa Idara ya Famasi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha huduma tabibu za kifamasia katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Bw. Soud Nasoro Soud ametoa wito kwa Wafamasia wote nchini kuzingatia miiko na maadili ya viapo vya taaluma ya Wafamasia ili kuhakikisha hakuna changamoto inayompata mgonjwa kwenye suala la upatikanaji wa huduma ya dawa katika  vituo vya kutolea huduma.

Kwa upande wake Bw. Athanas Macheyeki ambae ameenda kupata huduma ya dawa katika famasi iliyopo katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuendelea kuboresha huduma hasa katika upatikanaji wa dawa ili wananchi waweze kusaidika kupata huduma kwa urahisi.

"Kwakeli naipongeza sana Serikali chini ya mama yetu Rais. Dkt. Samia Suluhu Hasaan kwa kuwajali wananchi wake kwa upatikanaji wa huduma kwa haraka hasa katika eneo la upatikani wa dawa akisaidiwa na wasaidizi wake akiwemo Waziri Ummy Mwalimu ambaye ni Waziri wa afya."



 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...