Mwananchi apewa masaa 24 kuhama mtaa kisa kupora maeneo ya wenzao
Njombe Steven Kajula mkazi wa mtaa wa Lunyanywi halmashauri ya mji wa Njombe amepewa masaa 24 na wananchi wa mtaa huo kuhama kwenye mtaa wao wakidai ameshiriki kuvamia maeneo yao yenye mgogoro katika mtaa wa Yelusalemu na kuuza viwanja zaidi ya 42 bila ridhaa yao.


Uamuzi umetolewa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na diwani wa kata ya Mji Mwema Nestory Mahenge ambapo wamesema Kajula amekuwa akihatarisha usalama wao kwa kutishia wamiliki wa maeneo,Kutoa vibao vya zuio la kuuza viwanja hivyo vilivyowekwa na serikali ya mtaa sambamba na kutuma watu kwenda kuwashambulia wamiliki wanaopigania haki zao kuhusu viwanja hivyo.


"Nimepigwa na Kajula na wenzake nina alama hii,walikodi watu wakisema lazima niuawe naomba msichukulie mzaa hawa sio watu"amesema Lucy Kitavile huku Sabas Ndauka akisema kuwa "Wananchi wamechoka wamesema hatumuhitaji masaa 24 maana yake amekiuka taratibu na kanuni za nchi"


Diwani wa kata ya Mji mwema Nestory Mahenge amewaomba wakazi hao kupunguza hasira na kisha kumpa mwezi mmoja kufatilia kwa kina kuhusu mwananchi huyo pamoja na mwenyekiti aliyeshirikiana nae kuuza viwanja 42 ili taarifa zitakazopatikana zipelekwe kwa mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kwa ajili ya maamuzi kwa kuwa ndiye mwenye mamlaka ya kumuondoa mtu.

Hata hivyo baada ya mkutano huo watuhumiwa wanne akiwemo Steven Kajula wamegoma kuzungumza chochote kuhusu maamuzi yaliyotolewa na wananchi kwenye mkutano huo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...