Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Juni 15
VIFO
vya uzazi kwa mama Mkoani Pwani vimepungua kutoka vifo 96 kwa mwaka
2018 kati ya akinamama waliofika vituoni 43,488 hadi kufikia vifo 35
kwa mwaka 2022 kati ya akinamama 56,439.
Aidha Vifo vya watoto wachanga vimepungua kwa asilimia 5.5 kutoka 475 kwa mwaka 2018 na kufikia vifo 390 kwa mwaka 2022.
Hayo
yamebainika wakati Mkuu wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge
alipokuwa akizindua mpango wa mfumo wa m.mama Mkoani humo , ukumbi wa
wauguzi Kibaha Mjini,mfumo ambao utarahisisha masuala ya usafiri wa
dharura ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Alieleza
licha ya mafanikio na changamoto zilizopo, ujio wa mfumo wa m.mama
utaleta matokeo chanya katika kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Alielekeza kila mmoja kwa nafasi yake akatimize wajibu wake, ili kutekeleza mfumo huo.
"Mfumo
huu upewe kipaombele ,Nimpongeze Rais Samia Suluhu Hassan kwa m.mama
,maana inakwenda kunusuru maisha ya mama na mtoto,ni ibada,Twende
tukatimize wajibu wetu kufanikisha hili hadi ngazi za chini ,agizo la
Rais linahitaji utekelezaji, tutapimana kulingana na
utekelezaji,""Naamini Mkoa utafanya vizuri, alisisitiza Kunenge.
Hata
hivyo Kunenge alieleza, wakati ikizingumziwa m.mama inatakiwa iende
Sambamba na mkakati wa lishe, ili kuleta tija katika kuboresha huduma za
afya ya uzazi.
Awali
mganga mkuu wa mkoa wa Pwani dkt.Gunini Kamba anaeleza, changamoto
kubwa ni jiografia magari ya wagonjwa kutofika kwa wakati mama akipata
dharura lakini m.mama itakuwa mkombozi.
Alibainisha
vifo vya uzazi kwa mama na mtoto kwenye vituo mbalimbali vimeendelea
kupungua mwaka hadi mwaka kutoka mwaka 2018-2022.
"Kazi
bado ipo,jitihada ziongezeke ili kuendelea kupunguza idadi hii ya
vifo,kwani hakuna anaefurahi kupoteza mama ama mtoto wakati wa
kujifungua au kabla ya kujifungua " anasisitiza.
Gunini alisema,lengo ni kuondoa kabisa vifo vya mama na mtoto na kwa ujio wa m.mama malengo hayo watayafikia.
Akitoa
taarifa ya Hali Halisi ya viashiria vya huduma za afya ya uzazi mama na
mtoto ,Mratibu wa huduma za afya ya uzazi,mama na mtoto Mkoani Pwani,
Joyce alieleza utoaji huduma wa dharura umeongezeka kutoka vituo tisa
mwaka 2018 ambapo kwa mwaka 2022 vimefikia 23.
Pamoja na hayo alisema kwamba, vituo vya kutolea huduma ya afya vimeongezeka kutoka 300 na Sasa vipo 446.
Alieleza,
penye mafanikio hapakosi changamoto,kwani lipo tatizo la udumavu na
ukondefu kwani hali ya lishe,inachangia vifo vya uzazi kwa watoto na
mama ,ambapo ukondefu umeongezeka .
Alisema,
ukondefu umeongezeka kwa asilimia 7.2 kunatokana na ukosefu wa uhakika
wa chakula, magonjwa,malezi duni na uelewa mdogo wa lishe bora.
Akielezea
kuhusu utekelezaji wa Kitaifa wa huduma ya usafiri wa dharura (m.mama)
kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI dkt.Mshana alisema ni mfumo unaolenga
kutoa huduma ya usafiri kwa mama na mtoto kupunguza matatizo ya usafiri
wakati wa uzazi kwenda rufaa ili kuokoa maisha ya mama na mtoto kijumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...