WAZAZI wameaswa kuwalinda watoto dhidi ya matumizi mitandao huku wakiaswa kurejea kwenye malezi Kwa kuwafunza maadili mema ili waweze kujitegemea.

Wito huo umetolewa leo June 16, 2023 na Mgeni Rasmi na Afisa Tarafa Ukonga, Adrian Kishe wakati kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika ambayo hufanyika kila ifikapo Juni 16, kila mwaka na wakati wa kufunga kongamano la 26 lililoandaliwa na Chama cha Montesori Community of Tanzania (MCT) amesema watoto wanapaswa kupewa ulinzi na fursa katika malezi yao ili waweze kujengwa katika Hali ya kujitegemea maishani.

"Wazazi wenzangu niwakumbushe malezi ya watoto, unaompa mtoto simu ili asikusumbue ili wewe uendelee na majukumu yako, fuatilia Kwa makini kwenye hiyo simu mtoto anaangalia nini? siku hizi mitandao inakila kitu unaweza wewe kumpa Kwa mapenzi kumbe unampoteza." Amesema Kishe

Aidha kishe ameongeza kuwa jukumu la kumlinda mtoto ni la Kila mtu hivyo tunapaswa kuchukulia mtoto wa mwenzio ni wako unapaswa umlinde kumpenda na kumthamini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa MCT, Sarah Kiteleja  amesema kuwa mtoto anapaswa kufundushwa jinsi ya kujitegemea ili kumjenga na kumuandaa Kwa ajili ya Maisha yake ya baadae.

Aidha Sarah amesema kuwa wao kama Montessori wanajitahidi kumfundisha mtoto kujitegemea na kutatua changamoto zake mwenyewe pindi zinapojitokeza.

"Sisi tunahakikisha mtoto anaweza kujisimamia huku tukizingatia usalama wake ndio maana sisi tumekuja na kauli mbinu isemayo Mlezi Bora Kwa Malezi Bora"amesema.......

Siku ya mtoto Afrika huadhimishwa Kila mwaka ifikapo Juni 16 Kwa kukumbuka watoto zaidi ya 100 waliouwawa katika harakati za kutetea haki zao.

Kauli mbinu ya mwaka huu ya siku ya mtoto wa Afrika ikiwa ni "zingatia usalama wa mtoto dhidi ya digital"wakati MCT nao wamekuja na kauli mbinu ya "mlezi Bora Kwa malezi Bora tumpende.Tumlinde na tumthamini."
Picha za baadhi  wanachama cha Montesori Community of Tanzania (MCT) jijini Dar es Salaam leo Juni 16, 2023 wakati wa kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika na Kufunga Kongamano la 26 la chama hicho.
Mgeni Rasmi na Afisa Tarafa Ukonga, Adrian Kishe akizungumza na wanachama cha Montesori Community of Tanzania (MCT) jijini Dar es Salaam leo Juni 16, 2023 wakati wa kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika na Kufunga Kongamano la 26 la chama hicho.
 Hili ni kongamano la 26 ambao akizungumza na wanachama cha Montesori Community of Tanzania (MCT) jijini Dar es Salaam leo Juni 16, 2023 wakati wa kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika na Kufunga Kongamano la 26 la chama hicho.


Picha za baadhi  wanachama cha Montesori Community of Tanzania (MCT) jijini Dar es Salaam leo Juni 16, 2023 wakati wa kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika na Kufunga Kongamano la 26 la chama hicho.


Baadhi ya wanachama MCT, wakito burudani ya nyimbo na mashairi wakati wa kufunga Kongamano la 26 la wanachama cha Montesori Community of Tanzania (MCT) jijini Dar es Salaam leo Juni 16, 2023 na wakati wa kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika.




Matukio mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...